Wawakilishi walia Sheria ya Udhalilishaji kutumika kama kichaka cha kukomoana
Unguja. Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) imekiri sheria ya kuwanyima dhamana watuhumiwa wa udhalilishaji ina upungufu huku wananchi wakiitumia kama kichaka cha kukomoana. Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais, Sera, Uratibu na Baraza la Wawakilishi, Hamza Hassan Juma amesema wakati mwingine watu wanakuwa na ugomvi wa kawaida mtaani, lakini wanatumia…