Ukatili dhidi ya watoto wapungua Tanzania – Utafiti
Dar es Salaam. Matokeo ya utafiti wa kitaifa wa ukatili dhidi ya watoto na vijana (VACS-2024) yameonyesha ukatili kwa kundi la watoto kati ya miaka 13 hadi 24 umepungua kwa kiwango kikubwa. Matokeo hayo yameonyesha ukatili wa kingono, kimwili na kihisia kati ya watoto 11,414 umepungua ukilinganisha na utafiti wa kwanza wa VACS-2009 uliofanyika miaka…