Lema adai kuzuiwa Namanga, anyang’anywa hati ya kusafiria

Dar es Salaam. Mwanasiasa wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Godbless Lema anadaiwa kuzuiwa katika mpaka wa Namanga alikokuwa anafanya taratibu za kusafiri kwenda Nairobi nchini Kenya. Kwa mujibu wa Lema, safari yake kwenda jijini humo, ni kwa ajili ya kufanya matibabu ya maradhi yanayomsumbua, lakini alipofika mpakani akaambiwa hawezi kusafiri. Hata hivyo, ilidaiwa…

Read More

Makalla ajitoa ugomvi wa Makonda, Gambo

Arusha. Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Amos Makalla amesema hawezi kuingilia ugomvi kati ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Paul Makonda na Mbunge wa Arusha Mjini, Mrisho Gambo. Amesema viongozi hao wote ni wadogo zake na ni marafiki, hivyo anawatakia kila la heri katika mchakato unaofuata (ambao hakuutaja). Makalla…

Read More

PPRA wataja siri ya mafanikio ya utunzaji mazingira

Dodoma. Mamlaka ya Udhibiti wa Manunuzi ya Umma (PPRA) wametaja siri ya kupatiwa tuzo katika kilele cha siku ya Mazingira, wakigusia Mfumo wa Ununuzi wa Kidigitali (NeST), kwamba umekuwa mkombozi na unaendelea kuwabeba. Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi wa PPRA, Mkurugenzi wa Tehama, Michael Mushilo amesema mfumo wa NeST umeonyesha mafanikio, siyo kwa ajili ya…

Read More

Wanafunzi wote wenye sifa wachaguliwa kuendelea na masomo

Dodoma. Wanafunzi 149,818 sawa na asilimia 69.96 wamechaguliwa kujiunga na masomo ya kidato cha tano huku 64,323 wakichaguliwa kujiunga na vyuo vya elimu ya ufundi na ualimu katika mwaka huu. Idadi hiyo inafanya jumla ya wanafunzi 214,141 wakiwemo wasichana 97,517 na wavulana 116,624 waliokuwa na sifa za kuchaguliwa kujiunga na masomo ya kidato cha tano…

Read More

Nabi hajataka tamaa, atua tena Simba

Mambo ni moto! Siku chache baada ya nyota wa kimataifa wa Burkina Faso na Yanga, Stephanie Aziz KI kusajiliwa na Wydad Casablanca ya Morocco ni kama amefungua milango kwa mastaa wa Ligi Kuu Bara wanaowindwa na timu mbalimbali nje ya nchi. Wakati Aziz KI akijiandaa kushuka uwanjani nchini Marekani kukipiga dhidi ya Manchester City, Juni…

Read More

MWANDUMBYA ATETA NA UJUMBE WA KAMPUNI YA ALSTOM

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Bw. Elijah Mwandumbya, akiagana na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya ALSTOM, nchini Tanzania, inayojihusisha na uwekezaji katika ujenzi na uendeshaji wa miundombinu ya reli duniani,  Bi.  Kefilwe Mothupi, baada ya kumalizika kwa kikao kilichofanyika Ofisi za Wizara ya Fedha, Treasury Square, jijini Dodoma. Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Bw….

Read More