
UCHAMBUZI WA DANIEL MJEMA: Msichafuane ili kuongoza kura za maoni wala msichukue fomu kuuza sura
Kura ya turufu huwa inaweza kuzuia baadhi ya maamuzi yasitekelezwe, na hiki ndicho baadhi ya watia nia wa nafasi za ubunge na udiwani ama mawakala wao, wanatumia kuwapaka wenzao matope wakidhani ndio kete ya kuwasafishia njia. Lakini hatuhitaji watia nia ambao wanachukua fomu za kuomba kuteuliwa kuwa mbunge kwa kuongeza tu wasifu wake (CV), kuuza…