 
        
            Maji Ziwa Victoria kufanyiwa utafiti ubora wake
Mwanza. Kamisheni ya Bonde la Ziwa Victoria (LVBC) inatarajia kufanya utafiti wa maji ya Ziwa Victoria ili kujua ubora wake yanayotegemewa na watu milioni 45 kwa nchi za Afrika Mashariki. Utafiti huo unaofadhiliwa na Shirika la Maendeleo la Ujerumani (GIZ), utaanza hivi karibuni baada ya wataalamu kupewa mafunzo ya siku tatu ya namna ya kuufanya…
 
                         
                         
                         
                         
                         
                         
         
         
         
         
         
        