Mbili zabaki vita ya ubingwa ZPL, Mwenge yapumulia mashine
WAKATI ukibaki mzunguko mmoja wa kuhitimisha msimu huu wa Ligi Kuu Zanzibar (ZPL), timu mbili pekee zimesalia katika vita ya kuwania ubingwa, huku Mwenge ikiwa hatarini kushuka. Kwa sasa Mlandege inaongoza msimamo wa ligi hiyo ikiwa na pointi 59 sawa na KVZ inayoshika nafasi ya pili huku zikitofautishwa kwa mabao ya kufunga na kufungwa. Mlandege…