Kipigo chaishtua Srelio, yafuata mastaa DR Congo

BAADA ya Srelio kufungwa na Pazi kwa pointi 81-73 katika mchezo wa Ligi ya Kikapu Dar es Salaam (BDL), kocha wa timu hiyo, Miyasi Nyamoko amesema wameamua kuwaita nyota wawili kutoka DR Congo ili waje kuokoa jahazi. Katika michezo ya awali ya mashindano hayo iliyopigwa kwenye Uwanja wa Donbosco, Upanga, timu hiyo ilifungwa na Mchenga…

Read More

Mabadiliko makubwa yanukia Msimbazi | Mwanaspoti

VIKAO vizito vinaendelea ndani ya Simba kupitia tathimini za mchezaji mmoja mmoja kuona mchango wake kama utaisaidia timu hiyo msimu ujao 2025/26. Kuna kila mabadiliko makubwa yananukia kikosini Msimbazi huku majina kadhaa yakitajwa mpaka sasa. Tayari yapo majina ya mastaa wa kigeni waliokaliwa kooni kuhakikisha wanakatwa. Kati ya mastaa ambao ni 50 kwa 50 kusalia…

Read More

Mwanaharakati Kenya mbaroni akihamaisha kupingwa muswada wa fedha 2025

Nairobi. Wanaharakati nchini Kenya na Chama cha Mawakili Kenya (LSK) wamelitaka jeshi la polisi kumwachilia kwa dhamana mwanaharakati Rose Njeri ambaye alikamatwa na anaendelea kuwekwa kizuizini. Rose anashikiliwa kwa tuhuma za kutengeneza mtandao wa maoni na kuwashawishi Wakenya wenzake kushiriki katika hatua ya kupinga muswada wa fedha 2025. Njeri ambaye ni mfanyabiashara na mtaalamu wa…

Read More

Adebayor: Tulistahili fainali FA | Mwanaspoti

MSHAMBULIAJI wa Singida Black Stars, Victorien Adebayor amesema mechi mbili walizocheza dhidi ya Simba, waliwazidi wapinzani kiuwezo licha ya kupoteza mchezo wa kwanza kwa bao 1-0 na kwamba fainali ya Kombe la Shirikisho (FA) iliwastahili kwa namna walivyofunika Manyara. Singida ilianza kuvaana na Simba kwenye Uwanja wa KMC Complex, ikiwa ni kiporo cha Ligi Kuu…

Read More

Wabunge wacharuka gharama za vifurushi, matibabu ya figo

Dodoma. Bunge limepitisha bajeti ya Wizara ya Afya kwa mwaka 2025/26, huku mjadala kwa wabunge ukiwa kwenye gharama za vifurushi vya bima ya afya na matibabu ya ugonjwa wa figo. Wizara ya Afya ililiomba Bunge kuwaidhinishia Sh1.61 trilioni huku Sh991.75 bilioni kati ya hizo zikienda katika miradi ya maendeleo. Akichangia katika mjadala huo leo Jumanne…

Read More

MBUNGE NDULANE ASHAURI MAMBO SITA WIZARA YA AFYA

Na Janeth Raphael MichuziTv -Bungeni Dodoma MBUNGE wa Kilwa Kaskazini,Francis Ndulane (CCM) ameshauri mambo sita kwa Wizara ya Afya ikiwemo kupeleka Huduma za kupima magonjwa mbalimbali kwa kutumia Mashine za kisasa za CT Scan na MRI katika ngazi za Mikoa na wilaya. Akichangia mjadala wa makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara ya Afya leo…

Read More

Coastal Union kung’oa chuma Kagera

WAKATI Kagera Sugar, ikijiuliza inarudije chini kucheza ligi ya Championship, baada ya kushuka daraja Coastal Union, inataka kuongeza maumivu kwenye kidonda ikimtaka beki wao wa kati. Coastal Union inapambana kuinasa saini ya beki wa Kagera Sugar, Mohammed Salum aende kuongeza nguvu kwenye kikosi chao. Taarifa kutoka ndani ya Coastal Union ni kwamba, beki huyo amependekezwa…

Read More

Majaliwa aonya dhidi ya chokochoko za kisiasa

Dar es Salaam. Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa ametoa wito kwa vijana wa Tanzania kutojiingiza katika ajenda za watu wachache wanaolenga kuvuruga amani ya nchi, hususan kipindi cha kuelekea uchaguzi mkuu. Amesisitiza umuhimu wa vijana kuwa makini na kujiuliza kwa nini chokochoko huibuka mara kwa mara kila unapokaribia mwaka wa uchaguzi. Akizungumza leo, Juni 3, 2025…

Read More