RC Mtambi: Achaneni na imani za kishirikina machimboni

Musoma. Mkuu wa Mkoa wa Mara, Kanali Evans Mtambi amewataka wachimbaji wa madini hasa wadogo kuepuka kufanya shughuli zao kwa kutegemea imani za kishirikina badala yake wafanye kisayansi na teknolojia ili kupata tija zaidi. Kanali Mtambi ametoa agizo hilo leo Jumatatu Juni 2, 2025 alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusu kongamano na maonyesho ya…

Read More

KKKT kufanya harambee ujenzi kituo cha kulea watoto wenye usonji, Rais Samia mgeni rasmi

Dar es Salaam.  Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), limetangaza kuanza ujenzi wa kituo kipya cha watoto wenye usonji katika eneo la Kitopeni Bagamoyo mkoani Pwani. Usonji, au Autism Spectrum Disorder (ASD) ni hali ya ukuaji wa ubongo inayojumuisha changamoto katika maeneo ya mwingiliano wa kijamii, mawasiliano na tabia zinazojirudia. Hali hii inahitaji uangalizi…

Read More

LIVE: Kesi ya Lissu mubashara, mahakama kupokea ushahidi

Dar es Salaam. Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu leo Jumatatu Juni 2, 2025 inaanza kupokea ushahidi wa Serikali katika kesi ya kuchapisha taarifa za uongo mtandaoni, inayomkabili Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Tundu Lissu. Katika kesi hiyo inayosikilizwa na Hakimu Mkazi Mwandamizi, Geoffrey Mhini, Lissu anakabiliwa na mashtaka matatu ya kuchapisha mitandaoni…

Read More

Othman: Haijalishi tumeumizwa kiasi gani, tutaingia kwenye uchaguzi

Unguja. Mwenyekiti wa Chama cha ACT Wazalendo Taifa, Othman Masoud amesema haijalishi wamepitia magumu kwa kiasi gani kipindi kilichopita, lakini kamwe hawatasusia uchaguzi licha ya kuwapo dalili za kutaka kuwakatisha tamaa. Othman ambaye pia ni Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, amesema kwa namna yoyote itakavyokuwa watahakikisha wanapigania mifumo kabla ya uchaguzi lakini wasitarajie…

Read More

Sababu daraja la Tanzanite kutumiwa bure

Dodoma. Mbunge wa Muleba Kusini (CCM), Dk Oscar Kikoyo ameitaka Serikali kuanza kutoza fedha kwa watumiaji wa daraja la Tanzanite kama ilivyo kwa la Mwalimu Julius Nyerere. Dk Kikoyo amesema hayo bungeni leo Jumatatu Juni 2,2025 alipouliza swali la nyongeza ambapo amehoji kwa nini watumiaji wa daraja la Tanzanite wana uwezo lakini hawalipi, wakati daraja…

Read More

Rufaa waliotumwa na afande kusikilizwa kesho

Dodoma. Rufaa dhidi ya adhabu ya kifungo cha maisha gerezani  iliyotolewa kwa washtakiwa wanne waliokutwa na hatia kwenye  kosa la kubaka kwa kikundi na kumwingilia kinyume na maumbile binti Mkazi wa Yombo Dovya jijini Dar es salaam,  aliyetambulishwa mahakamani  kwa jina la X itaanza kusikilizwa kesho Juni 03, 2025. Wakata Rufaa katika kesi hiyo ni aliyekuwa…

Read More