Waliofaulu usaili Jeshi la Polisi waitwa kuripoti

Dar es Salaam. Jeshi la Polisi Tanzania limewataka vijana waliochaguliwa kujiunga nalo kuripoti katika Shule ya Polisi Moshi kuanzia Juni 12 hadi 14, 2025 kwa ajili ya kuhudhuria mafunzo. Vijana hao, ni wale waliofanya maombi na kufaulu katika usaili uliofanyika katika maeneo mbalimbali nchini. Taarifa ya wito huo, imetolewa jana Jumapili Juni 1, 2025 na…

Read More

SHIRIKA LA WAYDS LAANDAA MKUTANO WA AFYA (TANZANIA MENTAL HEALTH SUMMIT 2025) MKOANI SHINYANGA KWA KUSHIRIKIANA NA WIZARA YA AFYA

 Shirika la WAYDS limeandaa mkutano wa Afya Tanzania (TANZANIA MENTAL HEALTH SUMMIT 2025) utakayofanyika hapa Kahama mkoani Shinyanga kwa kushirikiana na Wizara ya Afya, Hospital ya Taifa ya Milembe, Foundation Botnar, Vitol Foundation, Doctor with Africa(CUAMM). Mkutano huu amabao una kaulimbiu “HATUA SHIRIKISHI NA JUMUISHI: KUKUZA USHIRIKIANO KATIKA AFYA YA AKILI KWA MAENDELEO ENDELEVU”, ukiwa…

Read More

Matarajio ya Watanzania bajeti ya afya ikisomwa leo

Dar es Salaam. Bajeti ya Wizara ya Afya kwa mwaka 2025/26 inawaslishwa leo Jumatatu, Juni 2, 2025 bungeni, huku macho ya Watanzania yakisubiri kuona Serikali inakuja na mikakati gani kuhakikisha inapambana na kuondoka kwa ufadhili wa Shirika la Maendeleo ya Kimataifa (USAID) nchini ambayo imefadhili sekta hiyo kwa miaka mingi. Ufadhili wa USAID ulisaidia maeneo…

Read More

Fedha zavuruga vigogo serikalini | Mwananchi

Dar es Salaam. Kuna nini bungeni? Ni swali linaloakisi hisia za watu wengi wanaoshangazwa na wimbi la Watanzania wanaojitokeza kuwania ubunge katika chaguzi za miaka ya karibuni. Ugumu wa swali hilo, unatokana na kwamba, ubunge umekuwa ndoto sio tu za wasio na ajira, bali hata viongozi wakiwamo wakuu wa mikoa, wilaya na wakuu wa taasisi…

Read More

Hili hapa Chama la Baum Ujerumani

WIKI zilizopita RB Leipzing ilimtambulisha kiungo Lisa Baum ambaye ana asili ya nchi mbili Tanzania na Ujerumani. Baum ambaye mara kadhaa aliwahi kusema anatamani kuitumikia timu ya taifa ‘Twiga Stars’ alijiunga na chama hilo akitokea Hamburger SV ya Ujerumani. Katika misimu miwili aliyoitumikia Hamburger SV ya Ligi daraja la kwanza alifunga mabao 10 kwenye mechi…

Read More

Mkongwe wa siasa, rafiki wa Mwalimu Nyerere afariki dunia

Dar es Salaam. Mwanasiasa mkongwe na shujaa wa harakati za uhuru wa Tanganyika, Alhaj Mustafa Mohamed Songambele, amefariki dunia siku chache baada ya kutimiza umri wa miaka 100, akiwa ameacha historia ya kipekee, ikiwemo kumbukumbu ya kumchekesha Mwalimu Nyerere hadi kudondoka sakafuni kwa kicheko. Alhaj Songambele, amefariki dunia usiku wa kuamkia leo Juni Mosi, 2025…

Read More

Pak Stars, Gymkhana zafunika daraja la tatu

KUPUNGUA kwa mvua jijini Dar es Salaam kumeamsha tena moto wa kriketi ambao umezileta ligi tatu tofauti katika viwanja vya Gymkhana, Leaders Club na Anadil Burhan, Ligi ya TCA-Diwa kwa wanaume, Ligi ya kufuzu michuano ya Caravans na Ligi B ya TCA kwa wanaume ndizo zilizoipamba kriketi mwishoni mwa juma. Timu zilizotoka kifua mbele ni…

Read More

Kesi ya Lissu kurushwa live, mahakama kupokea ushahidi

Dar es Salaam. Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu leo Jumatatu Juni 2, 2025 inaanza kupokea ushahidi wa Serikali katika kesi ya kuchapisha taarifa za uongo mtandaoni, inayomkabili Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Tundu Lissu. Katika kesi hiyo inayosikilizwa na Hakimu Mkazi Mwandamizi, Geoffrey Mhini, Lissu anakabiliwa na mashtaka matatu ya kuchapisha mitandaoni…

Read More

Clara awavuruga mabosi Al Nassr

MOTO wa mshambuliaji wa Kitanzania, Clara Luvanga unazidi kuwachanganya viongozi wa Al Nassr ya Saudia na inaelezwa wako kwenye mchakato wa kumboreshea mkataba wake uliosalia mwaka mmoja. Kwa sasa nyota huyo mwenye makombe mawili ya Ligi Kuu ya Wanawake Saudia yuko nchini kwenye majukumu ya timu ya taifa, Twiga Stars ambayo iko Dar es Salaam…

Read More