
Watuhumiwa wanane wa unyang’anyi wakamatwa Zanzibar
Unguja. Jeshi la Polisi Mkoa wa Mjini Magharibi linawashikilia watu wanane kwa tuhuma za kujihusisha na matukio ya unyang’anyi, kati ya hao watatu walijihusisha na tukio la hivi karibuni lililosambaa katika picha mjongeo mitandaoni. Picha hiyo ilionyesha mtu mmoja akivamiwa na kundi la watu waliovaa mavazi meusi ya mabaibui, wakiwa na silaha za mapanga na…