Singida Black Stars katikati ya mtego

MICHUANO ya Kombe la Shirikisho (FA), imefikia patamu ambapo tumeshuhudia timu mbili zikikata tiketi ya kucheza fainali, ikianza Yanga iliyoichapa JKT Tanzania mabao 2-0, kisha Singida Black Stars ikafuzu pia kibabe kwa kuicharaza Simba 3-1. Ushindi wa Singida ni wa kisasi baada ya kikosi hicho kupoteza mechi mbili za Ligi Kuu Bara, ikianza na kuchapwa…

Read More

Vyama vya siasa 14 vyatoa tamko kuhusu INEC, ZEC

Dodoma. Vuguvugu la uchaguzi mkuu nchini linaendelea kupamba moto, ambapo vyama 14 vya siasa vya upinzani vimeungana na kuunda jukwaa maalumu kwa lengo la kuwasisitizia Tume Huru ya Uchaguzi (INEC) na Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC),  kuwataarifu na kutangaza wagombea watakaoshinda katika Uchaguzi Mkuu unaokuja. Mbali na hayo, vyama hivyo vimesema kuwa vinaendelea na…

Read More

Kwa siku 10 kuanzia leo, hali ya hewa itakuwa hivi

Dar es Salaam. Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imetoa mwelekeo wa hali ya hewa kwa siku 10 kuanzia leo Jumapili, Juni 1, 2025, ikieleza uwepo wa mvua zinazoambatana na ngurumo za radi zinatarajiwa kunyesha baadhi ya maeneo ya nchi. Mvua hizo zinatarajiwa katika mikoa ya Kanda ya Ziwa Victoria, ikiwemo Kagera, Geita, Shinyanga,…

Read More

Watu 16,000 walivyotazama ‘Live’ mahubiri ya Askofu Gwajima

Dar es Salaam. Ama kweli Askofu Josephat Gwajima ni kiboko, ni maneno unaweza kuyatumia kuelezea namna watazamaji 16,000 walivyojitokeza kusikiliza mbashara (Live), mahubiri yake ya leo Jumapili Juni mosi, 2025 jijini Dar es Salaam. Idadi hiyo ni ya wale tu waliokuwa wakitizama ‘Live’ muda ambao Askofu Gwajima alizungumza kupitia runinga ya Rudisha TV, idadi inayotarajiwa…

Read More

Wanafunzi wa Tanzania wang’ara shindano la Tehama China

Dar es Salaam.  Wanafunzi wa vyuo vikuu vya Tanzania na wakufunzi wameibuka washindi katika Shindano la Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (Tehama) linaloendeshwa na kampuni ya teknolojia nchini China, Huawei.  Fainali hizo za kimataifa kwa mwaka 2024/25 zilifanyika mjini Shenzhen, China huku wanafunzi kutoka Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam (DIT), Chuo Kikuu cha Dar…

Read More

Kisa Yanga, maafande Tanzania Prisons waitana fasta

Wakati Tanzania Prisons ikiingia kambini leo Jumapili kuendelea na mazoezi kwa ajili ya mechi zilizobaki kukwepa presha ya play off, viongozi wameamua kuitana haraka kuimaliza Yanga. Maafande hao hawapo sehemu nzuri wakiwa na pointi 30 katika nafasi ya 13, wanatarajia kushuka uwanjani Juni 18 kuikaribisha Yanga yenye pointi 73 na inayohitaji ushindi kujiweka pazuri kutetea…

Read More

TZ Green yaanza kibabe TCA Majaribio

BAADA ya kupoteza mara nyingi dhidi ya TZ Blue katika mechi za majaribio kwa ajili ya kusaka kikosi cha timu ya taifa ya kriketi, TZ Green, hatimaye imeweza kufuta uteja baada ya ushindi wa mikimbio 32 kati mechi ya kwanza katika Uwanja wa UDSM mwishoni mwa juma. Wachezaji nyota  wa kriketi wamejigawa katika timu za…

Read More

Tanzania kuja na mtandao mmoja wa simu ndani, nje

Dar es Salaam. Wakati Tanzania ikiwa mbioni kuandaa mwongozo na sheria ya mtandao mmoja wa laini za simu ‘National Roaming’, Afrika imeweka makubaliano ya kuwa na matumizi ya mtandao mmoja ili kuingia kirahisi katika uchumi wa kidijitali. Mtandao mmoja wa laini za simu, utamwezesha mtumiaji kupata mtandao eneo lolote atakalokuwa hata kama hakuna mnara wa…

Read More