
Swissport Tanzania yatangaza faida ya Sh8.6 bilioni
Dar es Salaam. Kampuni ya huduma za usafiri wa anga nchini Tanzania, Swissport Tanzania PLC, imetangaza kupata faida kabla ya kodi ya Sh8.6 bilioni kwa mwaka wa fedha uliomalizika Desemba 31, 2024. Hayo yamebainishwa na Kaimu Ofisa Mtendaji Muu wa Swissport Tanzania PLC, Shamba Mlanga katika Mkutano Mkuu wa 40 wa mwaka wa wanahisa uliofanyika…