NIKWAMBIE MAMA: Uchaguzi si ngoma ya lelemama
Muda unakwenda bila kurudi nyuma. Hili ni jambo mahususi kwa Watanzania kukumbuka hasa katika kipindi hiki tunachouelekea uchaguzi mkuu. Uchaguzi si lelemama, ni mchakato unaoweza kutupatia viongozi au kutubadilishia kabisa maisha yetu kama Watanzania. Kuna baadhi ya majirani zetu wanaomba muda ungejirudia kabla hawajafanya chaguzi ili warekebishe mambo, lakini maziwa yakishamwagika huwa hayazoleki. Wenzetu wanajutia…