Kama wakwezo wanga, wazazi wako nao wanga
Canada. Ni mara ngapi umesikia malalamiko na tuhuma za uchawi katika baadhi ya familia za wanandoa wawe wanaokuhusu au kutokuhusu? Huwa unajisikiaje na kuelewaje? Si jambo jipya kusikia fulani akilalamika kuwa wakwe zake ni wanga. Mara nyingi, malalamiko haya hutolewa na wakamwana wanaposhindwa kuelewana na mama wakwe hata baba wake zao. Je, malalamiko haya yana…