Wawakilishi watakiwa kuendelea kudumisha amani, utulivu
Unguja. Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Hemed Suleiman Abdulla amewataka wajumbe wa Baraza la Wawakilishi kuendelea kudumisha amani na utulivu katika majimbo yao wakati na baada ya uchaguzi mkuu unaotarajia kufanyika Oktoba mwaka huu. Pia, amesema Serikali haitamvumilia mtu au kikundi, taasisi na chama chochote cha siasa, kitakachoashiria uvunjifu wa amani huku akisisitiza…