
Yanga yaoga minoti Zanzibar, yazawadiwa Sh100 milioni
Rais wa Zanzibar, Dk Hussein Ali Mwinyi ameizawadia klabu ya Yanga Sh100 millioni kwa kutambua ushindi na mafanikio makubwa ya klabu hiyo kwa msimu wa 2024/25. Zawadi hiyo ameitoa leo Jumatatu 30, 2025 wakati alipokutana na viongozi na wachezaji wa timu hiyo Ikulu kwa ajili ya kukabidhiwa makombe matano waliyotwaa msimu huu. …