……….
MKuu wa mkoa wa kagera, mhe Hajjat Fatma Mwasa Leo julai 1,2025 amezungumza na watanzania kupitia mkutano wa waandishi wa habari jijini Dodoma Kuhusu mafanikio ya serikali ya awamu ya sita katika mkoa huo.
Ambapo ndani ya uwasilishaji wa mafanikio hayo amegusia kuhusu kuanzisha kampeni maalumu ya kuhamasisha wananchi kula mlo kamili kwa kutumia vyakula vinavyopatikana katika mazingira yao. ili kupunguza tatizo la Udumavu kwa watoto ambalo limeshika kasi kubwa mkoani humo.