Majaliwa aliwaweka matumbo joto wazembe na wabadhirifu

Dodoma. Wakati Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitangaza kuwa hatagombea tena kiti cha ubunge, aliwaweka matumbo  joto wazembe na ubadhirifu.

Uamuzi wa Majaliwa kutogombea umetangazwa leo Jumatano, Julai 2,2025 zikiwa zimepita siku saba tangu ahutubie hotuba yake ya mwisho kwa wabunge akiwaomba wananchi wa Ruangwa kujiandaa akisema anakwenda kuchukua fomu.

Kutogombea ubunge kutahitimisha his-toria ya Majaliwa katika kiti cha Waziri Mkuu na kufanya Bunge la 13 lipate jina jipya la Waziri Mkuu.

Moja ya vitu vitakavyokumbukwa hasa kwa wale watakaopata nafasi ya kurudi tena katika Bunge lijalo, ni aina ya upole na ukaribu wake.

Majaliwa wakati wote alizungumza na kila mbunge aliyehitaji kubadilishana naye jambo bila kujali ametoka upande upi.

Mara nyingi Spika wa Bunge, Dk Tulia Ackson alikuwa akilalamika kuhusu wabunge kutumia muda mwingi wanapokuwa kwenye kiti cha Waziri Mkuu hata kufanya ashindwe kusikiliza jambo lililokuwa linaendelea ndani ya ukumbi wa Bunge.

Spika alilazimika kuwapangia muda maalumu wa kila mbunge anapotaka kukaa kwenye kiti cha Waziri Mkuu kwamba, isizidi dakika tatu lakini jambo hilo ni kama lilipuuzwa.

Katika Bunge la 11 lililokuwa na wabunge wengi kutoka vyama vya upinzani, Majaliwa hakuwahi kukutana na kashikashi kubwa kama ilivyowahi kutokea kwa mtangulizi wake (Mizengo Pinda) aliyewahi kukutana na mtiti wa kutaka kupigiwa kura ya kutokuwa na imani naye.

Alikuwa bingwa wa kujibu maswali

Kingine kitakachokumbukwa ni uhodari wa kujibu maswali ya papo kwa hapo kutoka kwa wabunge kila Alhamisi huku akijipambanua anaijua Tanzania kila ko-na.

Mara nyingi wabunge wa pande zote walikuwa wakiridhishwa na majibu ya Majaliwa na alitoa maelekezo na kufu-atilia utekelezaji wake hadi ngazi ya chi-ni.

Kwa wabunge ndani ya ukumbi wa Bunge waliishi na Majaliwa kama rafiki, ndugu na kiongozi wao ambaye hakuwa na mipaka ya namna ya kumfikia na ma-ra nyingi walikuwa wakieleza namna anavyofikika kwa urahisi kiongozi huyo.

Watumishi wazembe kicheko

Unaweza kusema wazembe kwenye utumishi watakuwa na kicheko kutokana na ukweli kuwa, Majaliwa tangu ali-poteuliwa hajawahi kupoa wala kuwa na muhali na watu wa aina hiyo.

Katika hotuba zake nje na ndani ya Bunge na kwenye mikutano ya hadhara amekuwa mbogo wakati wote akikemea na ‘kuwatumbua’ wanaobainika kuwa na upungufu katika utendaji wao.

Baadhi ya maeneo ambayo ha-watamsahau ni wasimamizi waliojenga Chuo cha Veta Wilaya ya Uyui mkoani Tabora alioamua kumalizana nao baada ya kubaini wametumia Sh11 milioni kwa ajili ya kujenga kibanda cha mlinzi.

Majaliwa alimwagiza Kamanda wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambanana Rushwa (Takukuru) Mkoa wa Tabora Musa Chaulo kuwakamata na kuwahoji waliosimamia ujenzi huo kwa tuhuma za ubadhirifu wa fedha.

Waziri Mkuu alikasirishwa na matumizi mabaya ya fedha za umma akisema hai-wezi kuvumilika na mara nyingi amekuwa na uamuzi ya papo kwa hapo akitaka uwajibikaji na uaminifu.

Majaliwa pia aliwasimamisha kazi mara moja waliokuwa watumishi 11 jijini Do-doma kwa tuhuma mbalimbali ikiwamo ufujaji wa fedha na migogoro ya viwan-ja.

Mtifuano mwingine Majaliwa aliupeleka Mkoa wa Iringa Wilaya ya Kilolo ‘ali-kowatumbua’ watumishi wanne kwa uzembe uliosababisha upotevu wa dawa katika hospitali ya wilaya jambo linalotajwa kuwa alikomesha mzizi wa fitina na hadi leo, hospitali hiyo ni mi-ongoni mwa zinazosifika kwa uwajibika-ji wa watumishi wake.

Katika Hospitali ya Wilaya ya Kasulu walikutana na mkono wa kiongozi huyo baada ya hospitali kutajwa katika wizi wa dawa huku akiahidi uchunguzi zaidi kwa maduka ya dawa yaliyosadikika kununua dawa hizo.

Katika ziara alizokuwa anazifanya wengi walikuwa na hofu na mkono wake wa kushoto, wakisema akiingiza kwenye mfuko wa ndani wa koti au mfuko wa kushoto wa shati lake ilikuwa ni hatari zaidi kuliko maneno ambayo an-geyatamka kabla.

Majaliwa siku zote hufanya uchunguzi kabla ya kuibuka na jambo na kwenye takwimu huwa anatembea na kitabu kidogo (note book) ambacho kinakaa kwenye mfuko wa shati au koti, akifika mahali hupenda kukumbushia mambo ya nyuma kabla ya kuhoji kinachoen-delea.

Related Posts