BILIONI 41.628 KUBORESHA SEKTA YA AFYA KATAVI

::::::

Bilioni 41.628 zimetumika katika uboreshaji wa huduma ya Afya mkoani Katavi ambapo zimejenga majengo , ukarabati na ununuzi wa vifaa tiba .

Ametabainisha hayo   leo 3 julai  2025 jijini

 Dodoma  na mkuu wa mkoa wa Katavi Mwanamvua Hodha Mrindoko wakati akizungumza na waandishi wahabari  katika  kueleza mafanikio ya serikali  ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Samia suluhu hassan. 

Hata hivyo amesema   huduma ya kusafisha damu imeanzishwa na umekamilika kwa asilimia 100 na huduma zimeanza kutolewa,ujenzi wa jengo la huduma za dharura( EMD) ,ujenzi wa nyumba ya watumishi na jengo la wagonjwa mahututi.

Vilevile  ongezeko la zahanati kutokamwaka 2021 hadi 127 mwaka 2025 ambalo ni sawa na ongezeko la zahanati 47 na vituo vya Afya vimeongezeka kutoka 17mwaka 2021 hadi 28 mwaka 2025 sawa na ongezeko lavituo 11.



Related Posts