FCC YAENDELEA KUTIMIZA MAAGIZO YA RAIS SAMIA

 :::::

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Ushindani Nchini (FCC)Bi.Hadija Juma Ngasongwa amesema wawekezaji wa ndani ya nchi wanasimamiwa na sheria madhubuti zinazosimamia uwekezaji ili kusaidia kulinda na kuimarisha biashara zao.

Taarifa hiyo ameitoa leo Julia 4,2025 Jijini Dar es salaamu alipofanya ziara ya kutembelea banda la Wizara ya Viwanda na Biashara katika maonyesho ya 49 ya biashara maarufu kama sabasaba,nakubainisha kuwa FCC itaendelea kutimiza maagizo ya Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan katika kuimarisha hali ya biashara Nchini.

“Lengo la kuanzishwa kwa Tume ya Ushindani(FCC) ni kusimamia na kuhimarisha ufanyaji wa biashara nchini, kulinda walaji dhidi ya mienendo potofu ya hali ya ufanyaji biashara kati ya kampuni na kampuni,pamoja na kudhibiti bidhaa bandia.”amesema Bi.Ngasongwa 

Nakuongeza kuwa” lengo kubwa ni kuhakikisha wawekezaji ndani ya nchi waone kwamba kuna sheria madhubuti ambazo zitawalinda na kusimamia uwekezaji wao wanao ufanya.”

Amesema kuwa FCC inajivunia na kushukuru Serikali kuweza kutengeneza mazingira rafiki ya wawekezaji kuhakikisha kwamba mwekezaji wa ndani kuweza kupata fursa zinazopatikana na ufanyaji wa biashara na mazingira mazuri yaliyowekwa katika serikali yake.

Pia ameongezea kuwa kushiriki kwao katika maonyesho ya sabasaba ni fahari kubwa,huku akiwaomba wageni wanaopita kwenye maonyesho hayo kuchangamkia fursa za uwekezaji kwani kuna zaidi ya Makampuni 3000 yanayo patikana kwenye banda la Wizara ya Viwanda na Biashara viwanda.

Amesema kuwa mwekezaji Mwenye mtaji mdogo anaweza kupata fursa kuungana na mwekezaji mwenye kipato kikubwa au mwenye uwekezaji mkubwa na kuweza kuhimarisha biashara kwa pamoja.

Amebainisha kuwa kuna sheria ambayo ina thibiti bidhaa bandia,nakwamba ni kosa la jinai kujihusisha na bidhaa bandia hivyo wananchi wafike kwenye banda la Wizara hiyoili waweze kujua namna ya kutofautisha bidhaa bandia na bidhaa halisi kwa sababu kuna wataalamu wanatoa elimu elimu hiyo. 

Related Posts