MWENGE WA UHURU WAZINDUA KITUO CHA AFYA KIA HAI.

Mwenge wa Uhuru 2025 umezindua Kituo cha Afya Kia wilayani Hai mkoani Kilimanjaro kilichogharimu milioni 209.

Akizungumza kiongozi wa mbio hizo za Mwenge, Ismail Ali Ussi alisema kuwa, lengo la Serikali ni kuhakikisha huduma za Afya zinasogezwa karibu na Wananchi. 

Alitumia nafasi hiyo kuwaasa madaktari watakaotoa huduma katika kituo hicho kuzingatia mwongozo wa utoaji huduma ili wananchi waweze kunufaika na fedha zilizotolewa na serikali yao. 

Lengo la mradi huo ni kuboresha utoaji wa huduma za Afya kwa wananchi wa Kia na maeneo jirani kwa kuanzisha huduma bora za Afya ya Baba  Mama na Mtoto, kupunguza vifo vya uzazi.

Related Posts