Na Said Mwishehe, Michuzi TV.
WAZIRI wa Nchi,Ofisi ya Rais,Mipango na Uwekezaji Profesa Kitila Mkumbo amesema mtu yeyote anayedharua vyombo vya habari huyo ni ‘Mtu kumpuuza.’
Profesa Mkumbo ameyasema hayo leo Julai 8,2025 jijini Dar es Salaam alipokuwa akizungumza na Wahariri na waandishi wa habari akiwasilisha taarifa ya Dira 2050 inayotarajiwa kuzinduliwa Julai 17 mwaka huu, Jijini Dodoma.
Kabla ya kutoa kauli hiyo Profesa Mkumbo, Mhariri na Mwenyekiti Mstaafu wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), Absolom Kibanda kuelezea katuni iliyoko mtandaoni inayosema Waandishi wa Tanzania ni ‘Toilet Paper’ na hivyo kumuomba Waziri kutoa kauli .
“…Serikali tunathamini uwepo wa Media tena iliyo imara. Serikali tunapotaka kujipima na kujitazama tunajiangalia kupitia Media.”
Profesa Mkumbo amesisitiza lengo la Serikali ni kuona vyombo vya habari vinakuwa na uchumi imara na mkakati uliopo ni kuwa na haja ya kuviimarisha vyombo vya habari. “Tunataka kutoa ruzuku kwa ajili ya media na hili linatikana na dhamira njema kupitia Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2025/30.” amesema
Akieleza umuhimu wa vyombo vya habari, amesisitiza kuwa hata Ilani ya CCM tumeangalia media katika kuisaidia na tunaposema kusaidia vyombo vya habari haina maana ikupendelee.
“Tunataka kuwa na vyombo vya habari imara na vifanye kazi kwa kuzingatia ukweli,media inayosimamia misingi ya taaluma na sio kupendelea.”