Ushindani wa Ligi ya Kikapu Mkoa wa Dar es Salaam (BDL), ulihamia katika fainali ya mashindano ya Kombe la Taifa kati ya Dar es Salaam na Mara, ambapo ulitokana na ubora wachezaji wa timu zote mbili kutokana na jinsi walivyozoeana wakutanapo kwenye BDL.
Mara iliwakilishwa na mastaa kama Baraka Sabibi, Mussa Chacha wanaokipiga JKT ilhali Abass Omary, Mwinyi Pembe, Jonas Mushi, Evance Davies na Tyrone Edward wanaichezea Stein Warriors.
Nayo Dar es Salaam iliwakilishwa na Amin Mkosa pamoja Haji Mbegu wanaocheza Dar City, Elias Nshishi na Alinani Msongole wapo ABC, Jimmy Brown na Omary Ndula wanakipiga JKT huku Josephat Peter anaichezea Pazi.