DIRA 2050 YA TANZANIA TUITAKAYO IMEKAMILIKA,RAIS SAMIA KUIZINDUA JULAI 17

*Dk.Samia aingia katika historia ya kuandika dira isiiyokuwa na muelekeo wa Itikadi ya Chama

*Profesa Mkumbo ataja hatua kwa hatua jinsi mchakato ulivyofanyika hadi sasa

Na Said Mwishehe,Michuzi TV.

WAZIRI wa Nchi,Ofisi ya Rais ,Mipango na Uwekezaji Profesa Kitila Mkumbo amesema Rais Dk.Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuzindua Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050  ambayo itajulikana Dira 2050 ambayo Inatoa muelekeo wa Tanzania Tuitakayo Julai 17 mwaka huu.

Uzinduzi huo unatarajia kufanyika katika Ukumbi wa Jakaya Kikwete mjini Dodoma ambapo wadau mbalimbali wa maendeleo wanatarajia kushuhudia tukio hilo la kihistoria ya kuwa na Dira 2050 huku Rais Dk.Samia anakuwa Rais wa pili nchini kuandika dira ya maendeleo .

Akizungumza na Wahariri na waandishi wa habari nchini leo Julai 8,2025 jijini Dar es Salaam Profesa Mkumbo amesema anaujulisha umma kuwa Rais Dk.Samia Suluhu Hassan atazindua rasmi Dira ya Taifa ya Maendeleo yaani Dira 2050 ,siku ya Alhamis ya Julai 17,2025 .

“Katika mkutano wa tatu wa Dira utakaofanyika tarehe hiyo ya Julai 17,2025 ,Rais Dk.Samia atazindua dira 2050 katika Ukumbi wa Jakaya Kikwete Dodoma kuanzia saa tatu kamili asubuhi.Ni tukio muhimu na kubwa la kitaifa 

“Ni kwa mara ya pili nchi yetu inaandika dira ya Taifa ya Maendeleo ambayo ,ingawa huko nyuma,tulikuwa na dira ya Azimio la Arusha ambayo ilikuwa ni dira kamili ya kitaifa , tulikuwa na programu ya Chama Cha Mapinduzi ya miaka 15 kuanzia mwaka 2007 mpaka 2002

“Lakini hii ni dira ya pili ambayo haina muelekeo  wa kiitikadi ya chama,kwani dira zote zilizopita huko nyuma zilikuwa na muekekeo wa itikadi ya Chama,azimio la Arusha ilikuwa ni ya Chama cha Mapinduzi wakati wa chama kimoja na ile nyingine ilikuwa programu ya Chama cha Mapinduzi lakini dira ya kwanza ambayo haina muekekeo wa chama ni hii Dira 2050 ya mwaka 2025 hadi mwaka 2050.

“Rais Dk.Samia anakuwa wa pili kuandika dira ,wa kwanza alikuwa Benjamin Mkapa ambaye ni Rais mstaafu wa Serikali ya Awamu ya Tatu.Kwahiyo tunampongeza Rais Dk.Samia kwa kupata fursa hiyo na kupata heshima hiyo ya kuandika dira itakayoongoza nchi yetu kwa miaka 25.

Awali wakati akizungumza na wahariri na waandishi wa  habari kuhusu mchakato wa maandalizi ya dira ya Taifa ya Maendeleo ,Profesa Mkumbo amesema Desemba 9 mwaka 2024 alikutana na wahariri wa vyombo vya habari kwa ajili ya kutoa tarifa ya hatua ambayo imefikia katika maandalizi ya dira ya Taifa.

“Niliwapa taarifa kuwa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Dk.Hussein Mwinyi atazindua rasimu ya dira ya taifa ya maendeleo 2050  na tayari alishaizindua.Na leo Julai 8 ,2025 tumewaita tena ili kupitia kwenu kutaarifu umma tumefikia wapi katika maandalizi ya dira na hatua gani inafuata.

“Maandalizi ya ya dira yamepitia hatua muhimu 13 na kama mtakavyoona mpaka sasa tumeshapita hatua 12 imebaki hatua ya 13 katika maandalizi ya dira ya maendeleo ya taifa,”amesema Profesa Mkumbo.

 Akieleza zaidi amesema baadhi ya hatua hizo ilikuwa ni kuandaa na kuidhinishwa kile kinachoitwa miongozo ya 2050 na kwamba Aprili 3,2023 ,Makamu wa Rais Dk.Philip Mpango kwa niaba ya Rais Dk.Samia Suluhu Hassan alizindua rasmi mchakato wa kuanza kuandika dira .

Hivyo mchakato huo  ulianza Aprili 3 mwaka 2023 na hivyo Aprili 3 mwaka huu mchakato wa kuandika dira umetimiza miaka miwili na miezi minne na hatua ya tatu ilikuwa kuunda vyombo vya kitaasisi vya kusimamia uandishi wa dira.

Profesa Mkumbo amesema mchakato wa uandishi wa dira umepita katika hatua tatu,kwanza kulikuwa na sekretarieti ya kuandika dira. Chombo cha pili waliunda timu kuu ya kitalaam ya kuandika dira na chombo cha tatu ilikuwa kamati ya uongozi wa dira hiyo ambayo  ilikuwa chini ya Waziri Mkuu Dk.Kassim Majaliwa na Mwenyekiti Mwenza Makamu wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.

Pia hatua nyingine  ilikuwa ni kufanya tathimini ya utekelezaji wa dira ya ya taifa ya Maendeleo ya 2000-2025. “Mtakumbuka tangu mwaka 2000 Serikali na wadau wengine wa maendeleo walikuwa wakiongozwa na dira ya taifa ya 2000-2025 ,hivyo kabla ya kufanya uandishi ilikuwa lazima kufanya tathimini ya utekelezaji wa ile dira kuona mafanikio na changamoto.

“Kwahiyo ripoti ya taarifa hii ya tathimini imezinduliwa rasmi Desemba 9 mwaka 2023 kwenye mkutano wa kwanza wa kitaifa wa dira na mgeni rasmi alikuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.Samia Suluhu Hassan na kupitia mkutano ule  alizindua rasmi pia nyenzo ya kukusanya maoni ya wananchi na wadau Kuhusu dira ya taifa ya maendeleo 2050

“Kwahiyo mkutano wa kwanza ulifanyika Desemba 9 ukiwa na majukumu mawili ,kwanza kufanyika taarifa ya tathimini ya dira ya maendeleo ,lakini pili  Rais alizindua timu kuu ya kitalaam na akazindua nyenzo ya kukusanya maoni ya wadau.”

Akifafanua zaidi amesema hatua ya tatu ilikuwa kukusanya maoni ya wananchi na wadau wa maendeleo kuhusu matarajio yao ,maudhui gani yaingie katika dira ya 2050 na zoezi hilo lilikuwa pana na shirikishi likiwa limesambaa nchi nzima na limegusa kila mwananchi na kila mdau na wamefakia zaidi ya watu milioni 1.2

“Na sampuli kubwa katika tafiti huwa ni watu 5000 na wakizidi sana 10,000 lakini sampo nyingi ni 2000 au 3000 lakini mchakato huu wa dira ya maendeleo umewafikia watu zaidi ya milioni 1.2 na tulitumia njia saba ikiwemo kufanya tafiti tulifanya katika ngazi ya tawi.

Pamoja na hayo Profesa Mkumbo amesema hatua nyingine muhimu ambayo mchakato huo wa kuandaa dira umepitia pia ni mchakato wa maamuzi ndani ya Serikali na Juni 22 mwaka huu waliwafikisha kwenye baraza la mawaziri na likaidhinisha rasmi dira ya maendeleo .

“Kwahiyo Juni 22 mwaka 2025 ni siku muhimu sana kwasababu ni siku ambayo baraza la mawaziri lilipitisha rasmi dira ya Taifa ya maendeleo na baada ya hapo ikahamia katika hatua nyingine kutoka Serikalini na ikaenda katika Bunge na Bunge liliridhia

“Maana yake ni nini hapo tuseme hii dira ambayo inaisha muda wake iliidhinishwa na baraza la mawaziri  ikaisha hapo na wala haina tatizo wala haina kosa lakini mwaka huu Rais Dk.Samia aliagiza na kueleza lazima hii dira iende Bungeni lengo lake ni kuweka ulinzi 

“Dira hii itatekelezwa na marais wasiopungua watatu mpaka wa nne ,Rais Samia anakuwa wa kwanza atajayeisimamia mpaka mwaka 2030 na Rais atakayekuja kama atakaa miaka 10 maana yake atatoka mwaka 2040 na Rais mwingine akikaa miaka 10 atatoka madarakani  mpaka 2050 ,kwa hiyo angalau marais wasiopungua watatu wataisimamia dira 2050.

“Tuliamua kupeleka Bungeni na Rais alifanya uamuzi sahihi lengo ni kuweka ulinzi,ikiishia kwenye baraza la mawaziri ikienda bungeni ukitaka kitu chochote kubadilisha ambacho kimefika Bungeni lazima urudishe huko.

“Kwahiyo tumeweka ulinzi mkubwa na ukija hapa ukawa Rais ukasema hutekelezi dira lazima uende Bungeni ukawishi Bunge kwa niaba ya wananchi.Kwahiyo ilikuwa hatua kubwa ,”amesema.

Hivyo amesema hatua ya mwisho ambayo ndio hiyo iliyobakia ni kuutaarifu umma wa Watanzania kupitia wahariri na waandishi wa habari mchakato wa maandalizi ya dira ya maendeleo umekamilika na sasa wanayo dira ya Taifa ya maendeleo itakayojulikana kama Dira 2050 na itajulikana hivyo kwa kiswahili na kingereza.“Kwahiyi hatutakuwa na tafsiri ya dira ,hakuna vision 2050.”

Ameongeza Dira hiyo itaitwa Dira 2050,kwahiyo itakuwa hivyo na ndio tutambea nayo kwa miaka 25 ijayo .Kwahiyo anautangazia umma ujue wanayo dira ya maendeleo ambayo inaitwa Dira 2050 .

Related Posts