Jesca avunja rekodi ufungaji | Mwanaspoti

Mchezaji wa JKT Stars na timu ya wanawake ya Mkoa wa Dar es Salaam, Jesca Ngisaise amevunja rekodi ya kufunga pointi nyingi peke yake, ambapo alivuka kiwango kilichozoweleka cha pointi zisizozidi 50 kwa mchezo ambacho mastaa wengi hufikia.

Hata hivyo, katika mashindano Taifa alifunga pointi 90 peke yake kati ya 172-58 walizoifunga Dodoma, huku mchezo mwingine aliofunga pointi nyingi ulikuwa dhidi ya Pwani aliotupia 56 ambao Dar ilishinda 108-43.

Jesca alifunga pointi 50 dhidi ya Mbeya ambao Dar ilishinda 112-22, ilhali alifunga 40 dhidi ya Unguja ambapo Dar es Salaam ilishinda kwa pointi 82-35.

Katika Ligi ya Kikapu Mkoa wa Dar es Salaam upande wa wanawake (WBDL), akiwa na JKT Stars alifunga pointi 60 dhidi ya  UDSM Queens ambao timu yake ilishinda 109-26 kisha akatupia 62 walipoifumua  Mgulani JKT kwa pointi 121-23 na kamaliza kwa kuifumua pointi 35 Reel Dream wakishinda 80-50.

Related Posts