…..,……,…..
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa ameagiza miradi yote mikubwa iliyojengwa na inayoendelea kujengwa kwa fedha za ndani zinazotokana na Kodi iandikwe ili kuwaonyesha Watanzania namna Kodi wanazolipa zinavyofanya kazi.
Waziri Mkuu ametoa maagizo hayo leo Julai 8, 2025 Jijini Arusha wakati akifungua kikao cha tathmini ya utendaji kazi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kwa mwaka wa fedha 2024/2025 na kuweka mikakati ya kufanya vizuri kwa mwaka wa fedha 2025/2026 ambapo TRA imewekewa lengo la kukusanya Sh. Trilioni 36.
Waziri Mkuu amesema katika baadhi ya miradi ikiwemo midogo imekuwa ikiwekwa majina ya wahisani huku miradi mikubwa iliyojengwa kwa Kodi ikiachwa likiwemo daraja la Kigongo – Busisi na kuwaelekeza wakuu wa mikoa kila mmoja kwenye eneo lake kuainisha miradi iliyojengwa kwa Kodi na kuweka Bango ili wananchi waone umuhimu wa kulipa kodi.
Aidha Waziri Mkuu ameielekeza Wizara ya Fedha kufanya mapitio ya Sera, kanuni na mifumo ili kuona kama ipo sehemu inayokwamisha utendaji kazi wa TRA irekebishwe ili kuboresha na kurahisisha utendaji kazi wake.
#KIKAO KAZI CHA TATHMINI YA UTENDAJI KAZI WA TRA 2024/2025