Coastal, Pamba zatua kwa Maseke

TIMU za Coastal Union na Pamba Jiji zimeingia anga za kuhitaji huduma za kipa Wilbol Maseke aliyemaliza mkataba wake na KMC msimu ulioisha akiwa na ‘clean sheet’ tatu alizozipata katika mechi tano alizocheza.

Awali Mbeya City ndiyo ilianza kusaka huduma ya kipa huyo, lakini haikufikia naye mwafaka na sasa timu ambayo inamwelekeo mzuri ni Coastal inayotarajia kutomuongezea mkataba Aaron Kalambo aliyemaliza mkataba wa miezi sita baada ya kusajiliwa dirisha dogo.

Chanzo cha ndani kutoka Coastal kilisema: “Kuna mabadiliko makubwa yatafanywa kuanzia kwa wachezaji hadi benchi la ufundi, ila kwa sasa ni mapema kulifafanua hilo.

“Kuna uwezekano mkubwa wa kuachana na Kalambo, hivyo lazima atasajiliwa kipa mwingine ambaye tutafikia naye dau, mwingine ambaye hataongezewa mkataba ni Erick Nkosi pia tuna mchakato wa kumtafuta kocha mkuu.”

Alipotafutwa Maseke izungumzia hilo alisema: “Itakuwa vigumu kusema ofa za timu ambazo nazungumza nazo kabla sijamalizana nazo. Kila kitu kikiwa tayari nitakuwa na uhuru wa kuongea.” Kipa huyo alitua KMC akitokea Azam na tayari keshamaliza mkataba nayo.

Related Posts