Ibenge amtibulia dili beki KMC

BAADA ya Azam FC kumtambulisha aliyekuwa kocha wa Al Hilal Omdurman ya Sudan, Florent Ibenge, inaelezwa kuwa dili la beki wa KMC, Raheem Shomari, limekufa baada ya kocha huyo kujiunga na Matajiri wa Chamazi.

Nyota huyo aliyeibuka Mchezaji Bora Chipukizi kwa msimu wa 2023-2024, alikuwa katika hatua za mwi-sho kumalizana na Al Hilal ya Sudan, lakini dili ni kama limebuma hivi.

Chanzo kiliiambia Mwanaspoti kuwa beki huyo chipukizi alikuwa chaguo la kocha Ibenge, hivyo viongozi wamejitoa kwenye mazungumzo na uongozi wa mchezaji.

Kiliongeza kuwa Ibenge ndiye aliyetoa pendekezo la kuwa naye msimu ujao, hivyo kujiunga Azam huenda akamhitaji kwani anaijua vyema Ligi Kuu.

“Nilivyosikia kwa sasa ni mchezaji huru, amemaliza mkataba na KMC, na kule kwa sasa hakuna kinachoendelea tena kati ya Hilal na uongozi wa mchezaji. Kocha aliyemtaka kaondoka, labda ata-kayekuja kama atamhitaji,” kilisema chanzo hicho.

Mwanaspoti tulipomtafuta Raheem alisema: “Unajua mimi siongei na timu, ni menejimenti yangu ndiyo inajua kila kitu, lakini dili lilikuwepo ila sijui kinachoendelea.”

Kama Ibenge atamhitaji beki huyo, basi huenda akakutana na Pascal Msindo ambaye amekuwa na ki-wango bora ndani ya misimu miwili mfululizo Azam. Hata hivyo, eneo la mlinzi wa kushoto ukimtoa Msindo ambaye pia anatajwa kuhusishwa na Simba hakuna beki mwingine  kwani miezi michache iliyo-pita waliachana na Msenegali Cheikh Sidibe.

Hivyo, kama Ibenge aliulizia huduma yake akiwa Sudan, itakuwa rahisi zaidi kwa sasa kutokana na kujiunga na Azam.

Related Posts