RAIS MSTAAFU JAKAYA KIKWETE ASHIRIKI MKUTANO WA JARIDA LA UONGOZI LA AFRIKA

 

Mheshimiwa Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, ameshiriki katika Mkutano Mkuu wa Afrika ulioandaliwa na Jarida la Uongozi la Afrika (African Leadership Magazine) na Taasisi ya Uongozi wa Afrika (African Leadership Organization) jijini London, Uingereza. 

Mkutano huo unazungumzia masuala mbalimbali ya Afrika, ikiwemo Uongozi, Uwekezaji na Ushindani wa Kimaendeleo kwa kauli mbiu ya: “Powering Leadership, Investment and Competitiveness”.

Awali, Mheshimiwa Rais Mstaafu ambaye ni Mwenyekiti wa Bodi ya Washauri ya African Leadership Organization (ALO), aliongoza vikao vya Bodi hiyo ambayo inaangazia masuala mbalimbali ya maendeleo ya Afrika kijamanii na kiuchumi. 

Bodi hiyo ina wajumbe kutoka nchi mbalimbali duniani, akiwemo Mhe. Dkt. Jewel Howard Taylor, Makamu wa Rais Mstaafu wa Liberia; Prof. Tahir Akhtar, Mkurugenzi wa Kampuni ya Adam Global Holdings UK/UAE; Dkt. Victor Oladukon, kutoka Benki ya Maendeleo Afrika (AfDB); Dkt. Christian Lindfeld, Mwanzilishi na Mkurugenzi Mtendaji wa Africa Ventures Advisory – Germany; Jenerali William Kip Ward, Kamanda Mkuu Mstaafu wa Kamandi ya Jeshi la Marekani barani Afrika; Mhe. Nomvula Makonyane, Makamu Katibu Mkuu wa ANC – Afrika Kusini; na Dkt. Ken Giami, Mtendaji Mkuu wa African Leadership Organization (ALO). 

Related Posts