Zanzibar yanadi maeneo sita ya uwekezaji

Dar es Salaam.  Wakati Zanzibar inajipanga kuwa kituo bora cha uwekezaji kwa wawekezaji wa ndani na nje ya nchi imeainisha ikiainisha sekta sita zenye fursa kubwa za ukuaji wa haraka zinazoweza kutumiwa na wawekezaji.

Sekta hizo ni uchumi wa buluu, utalii, mali isiyohamishika (real estate), viwanda, kilimo na ushirikiano kati ya sekta binafsi na ya umma (PPP).

Akizungumza katika Maonesho ya 49 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (DITF), Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum wa Zanzibar, Mwanaidi Ali Khamis, alifungua rasmi Zanzibar Business Day kwa ujumbe thabiti.

 “Zanzibar iko tayari kwa biashara na iko tayari kuvutia uwekezaji wenye uwajibikaji,” amesema.

Tukio hilo, lililoandaliwa kwa kaulimbiu ya ‘Zanzibar Ardhi ya Fursa za Uwekezaji’, lililenga kuonesha dira ya maendeleo ya muda mrefu ya visiwa hivyo na vipaumbele vya kisekta.

Kipaumbele kikubwa kiliwekwa kwenye sekta ya uchumi wa buluu huku maofiss wa serikali walieleza maeneo ya kimkakati ya uwekezaji katika sekta hiyo uvuvi na ufugaji wa samaki, utalii wa baharini, utafutaji wa mafuta na gesi, usafiri wa baharini, na upangaji wa matumizi ya bahari.

Katika uoande wa Uchumi wa Buluu na Uvuvi amesema jiografia ya Zanzibar  imezungukwa na maji inaweka vikwazo kwa kilimo kikubwa lakini inatoa fursa pana kwa sekta za kiuchumi zinazotegemea bahari.

“Tayari tumetoa mabwawa ya kufugia samaki na boti kwa wavuvi wa ndani kupitia fedha za mpango wa msaada wa Uviko-19 na waliopokea msaada huo sasa wanaendesha shughuli zao kwa mafanikio,” amesema.

Alibainisha kuwa boti moja hugharimu kati ya Sh15 milioni hadi Sh20 milioni, jambo ambalo ni gumu kufikiwa na watu wengi.

“Ndiyo maana tunahitaji wawekezaji,” amesema.

Sekta ya utalii iliendelea kutajwa kuwa uti wa mgongo wa uchumi wa Zanzibar, ikichangia takribani asilimia 30 ya Pato la Taifa huku maofisa wa serikali sasa wanataka kuboresha huduma na vivutio ili wageni wakae muda mrefu zaidi na kutumia fedha nyingi zaidi.

Maeneo matano ya kipaumbele yametambuliwa ambayo ni utalii wa urithi, michezo ya majini, utalii wa mikutano, utalii wa michezo (hasa kuelekea Kombe la Mataifa ya Afrika  Afcon) na utalii wa kiikolojia.

“Tunayo zaidi ya maeneo 87 ya kihistoria, lakini mengi yanahitaji ukarabati ili yaweze kutumika ipasavyo,” amesema.

“Kwa sasa watalii hukaa kati ya siku 7 hadi 8. Lengo letu ni kuboresha miundombinu na huduma za utalii ili wakae zaidi na kutumia zaidi.

Makazi na maendeleo ya mijini pia yalitajwa kuwa kipaumbele kingine Kwa mujibu wa Khamis Dunia kutoka Mamlaka ya Uwekezaji Zanzibar (Zipa), ni takribani asilimia 20 tu ya Wazanzibari wanaoweza kumudu nyumba kupitia soko rasmi la ardhi.

“Tunahitaji uwekezaji mkubwa katika makazi nafuu, na tunawakaribisha wawekezaji kusaidia kuziba pengo hili,” amesema dunia.

Mbali na makazi, dunia alitaja fursa za uwekezaji katika sekta za usindikaji wa mazao na kilimo. Serikali ya Zanzibar inatoa motisha mbalimbali kwa wawekezaji ii kuunga mkono ajenda yake ya uwekezaji.

Related Posts