Kumekucha Yanga, mastaa sita Kuachwa

BAADA ya Yanga Princess kuonyesha kiwango kizuri msimu huu, itaachana na wachezaji sita na kuongeza nyota wapya.

Nyota hao ni Danai Bhobho ambaye alitumikia Yanga kwa msimu mmoja akitokea Simba Queens, Rebeca Ajimida kutokea Nigeria ambaye hakupata nafasi ya kucheza kikosini hapo.

Neema Paul aliyemaliza mfungaji bora kikosini hapo akiweka kambani mabao 12 sawa na Jeaninne Mukandayisenga, Lucy Pajero, Winifrida Castory na Asha Omary ambao hawakupata nafasi ya kuanza kikosini.

Baadhi ya nyota wameanza kuhusishwa na timu zingine Neema inaelezwa Simba imeanza kuzungumza nae baada ya kumaliza mkataba na wananchi hao, Pajero tayari amejiunga na Mashujaa kwa mkataba wa mwaka mmoja na muda wowote atatambulishwa.

Asha ambaye kwa sasa yupo kwenye majukumu ya timu ya taifa ‘Twiga Stars’ inayocheza mashindano ya WAFCON nchini Morocco na alianza kwenye mechi dhidi ya Mali inaelezwa JKT iko kwenye mpango wa kumsaini pamoja na Castory ambaye tayari amesaini mkataba.

Related Posts