Lengo la Yanga CAF ni Hatua ya Makundi – Global Publishers



Rais wa Klabu ya Yanga SC, Eng. Hersi Said

Rais wa Klabu ya Yanga SC, Eng. Hersi Said, amesema kuwa malengo ya klabu hiyo kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika (CAF Champions League) kwa msimu ujao ni kuhakikisha wanatinga hatua ya makundi.

Akizungumza kuhusu maandalizi ya timu hiyo, Eng. Hersi alieleza kuwa baada ya kufanikisha usajili wa wachezaji wenye viwango vya juu, klabu itaweka mkazo katika kuijenga timu kwa ajili ya hatua za juu zaidi kwenye mashindano hayo.

“Kwa sasa malengo yetu ni kufika hatua ya makundi. Tukishafika hapo, upepo utabadilika kwa sababu wachezaji tuliowasajili wana uwezo mkubwa, hivyo tutawajenga zaidi kwa ajili ya hatua kubwa za kimataifa,” alisema Eng. Hersi.

Kauli hiyo imekuja wakati ambapo Yanga SC inaendelea na maandalizi ya msimu mpya, huku ikiwa na rekodi ya mafanikio makubwa msimu uliopita kwa kutwaa mataji matano, ikiwa ni pamoja na ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara.











Related Posts