Waziri wa Mambo ya Nje wa Cyprus Akamilisha Ziara ya Kikazi Nchini Tanzania

Waziri wa Mambo ya Nje wa Cyprus. Dkt. Constantinos Kombos amekamilisha ziara yake ya kikazi ya siku tatu nchini na kuagwa na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Said Shaib Mussa kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar Es Salaam Julai 10, 2025.

Wakati wa ziara yake nchini, Dkt. Constantinos Kombos alikutana na viongozi mbalimbali akiwemo mwenyeji wake, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Mahmoud Thabit Kombo ambapo kwa pamoja walisaini Hati ya Makubaliano Kuhusu Mashauriano ya Kisiasa kati ya Tanzania na Cyprus ambayo yanatarajiwa kukuza na kuimarisha uhusiano wa kidiplomasia na kiuchumi baina ya mataifa hayo mawili.












Related Posts