
July 11, 2025


Simba yafunga hesabu kwa Conte
Simba imefikia makubaliano ya kumsajili kiungo wa CS Sfaxien, Balla Moussa Conte leo Ijumaa, Julai 11, 2025. Kiungo huyo wa ulinzi raia wa Guinea mwenye umri wa miaka 21, alikuwa na mkataba wa mwaka mmoja na Sfaxien unaofikia tamati 2026 ambao Simba imeuvunja na kumnasa mchezaji huyo. Conte amekuwa miongoni mwa wachezaji tegemeo wa Sfaxien…

Latra, DCEA wawahimiza madereva, makondakta kutambua sheria ya dawa za kulevya
Dar es Salaam. Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (Latra) kwa kushirikiana na Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya nchini (DCEA), imewataka wamiliki wa magari ya usafiri wa abiria na mizigo kuhakikisha wanawaajiri madereva na makondakta wenye uelewa kuhusu Sheria ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya. Wito huo umetolewa Julai 11,…

Tanzania, China zabainisha mikakati kuimarisha elimu ya ufundi stadi
Dar es Salaam. Tanzania na China zimeeleza mikakati ya kuendelea kuimarisha ushirikiano baina yao katika maeneo matatu ikiwemo ubadilishanaji wa wakufunzi, wanafunzi na kuimarisha elimu ya kidigitali. Katika elimu ya kidigitali, China imesema itashirikiana na Tanzania kuandaa vitabu vya kidigitali vyenye lugha mbalimbali pamoja na kuhamasisha matumizi ya teknolojia hizo. Eneo la tatu la ushirikiano…

Nida kuja na mkakati wa kuandikisha watoto vitambulisho vya Taifa
Dar es Salaam. Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa nchini (Nida) imesema inaandaa mkakati wa kufanya utafiti ili kuanza kutoa vitambulisho vya taifa kwa watoto nchini. Hayo yamebainishwa na Ofisa Uhusiano wa Nida, Godfrey Tengeneza, alipozungumza na Mwananchi leo Ijumaa, Julai 11, 2025. Tengeneza amesema mamlaka hiyo imejipanga na ipo katika hatua za mwisho za kukamilisha…

Magonjwa haya yanasumbua Dodoma | Mwananchi
Dodoma. Wakati serikali na wadau wa afya wakiendelea kutoa elimu ya afya kwa wananchi namna ya kujikinga na magonjwa yasiyo ya kuambukiza, Mkoa wa Dodoma umetwajwa kuwa kinara wa magonjwa matatu ambayo ni macho, magonjwa ya akili na selimundu. Kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na wizara ya afya kwa kushirikiana na Hospitali ya rufaa ya…

Biashara ya Tanzania, India yafikia Sh20.64 trilioni, uwekezaji ukiongezeka
Dar es Salaam. Biashara kati ya India na Tanzania imeongezeka hadi kufikia Sh20.64 trilioni mwaka 2024, kutoka Sh20.13 trilioni mwaka uliotangulia huku ikiwa kinara kwa uwekezaji nchini kwa miaka mitano mfululizo. Kwa mujibu wa Balozi wa India nchini Tanzania, Bishwadip Dey, ongezeko hilo limetokana na kuimarika kwa uhusiano wa pande mbili na sera bora za…

Mataifa ya Afrika yatakiwa kuja na suluhisho utoshelevu wa chakula
Dar es Salaam. Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Stephen Nindi amezitaka nchi za Afrika kushirikiana na mataifa mengine kutengeneza suluhisho la utoshelevu wa chakula na kutafuta fursa za biashara. Kiongozi huyo amesema mustakabali wa kilimo cha Afrika utategemea Waafrika huku akitaja sekta hiyo kuwa inachukua nafasi muhimu katika uchumi. Kiongozi huyo wa Wizara…

betPawa yaandika historia ya ushindi mkubwa wa aviator Afrika wa Sh2.6 billion kwa raundi ya mchezo mmoja
Kampuni kinara ya michezo ya kubashiri mtandaoni barani Afrika, betPawa, imeitikisa Afrika na kutengeneza historia kufuatia ushindi wa Sh2.6 bilioni (sawa na Dola za Kimarekani milioni 1.1) katika raundi moja kupitia mchezo wa aviator maarufu kwa jina la kindege. Washindi walioshinda fedha hizo wanatoka nchi za Cameroon, Ghana na Zambia. Haya ni malipo makubwa zaidi…

RC CHALAMILA ATAKA WATAALAM KUJA NA SULUHU YA MSONGAMANO WA MAGARI DAR
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Albert Chalamila amewataka Wakuu wa wilaya za Ilala,Temeke na Kigamboni, wakurugenzi wa Halmashauri pamoja na wataalamu ndani ya Jiji hilo kuwa na ubunifu hususani kwenye kukabiliana na changamoto ya msongamano wa magari ili Jiji hilo liweze kuimarika kiuchumi na liendelee kuwa kivutio kwa wageni na watalii kutoka…