NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM
Ofisi ya Mwandishi Mkuu wa Sheria (OCPD) imetafsiri sheria 300 kati ya sheria 446 kutoka lugha ya kiingereza kuwa kiswahili katika kipindi cha miezi sita cha mwaka 2025 ambapo Sheria 146 zilizozobakia zinatarajiwa kutafsiriwa katika bajeti ya mwaka fedha 2025/2026 ili wananchi wanapozisoma wazielewe.
Ameyasema hayo leo Julai 11,2025 Waziri wa Katiba na Sheria Dkt. Damas ndumbaro alipotembelea banda la Ofisi ya Mwandishi Mkuu wa Sheria (OCPD) katika Maonesho ya kimataifa ya Biashara ya Dar es salaam (Sabasaba).
Aidha Dkt Ndumbaro amesema ofisi ya Mwandishi mkuu wa Sheria imekuwa msaada mkubwa kwa mahakama nchini kwa kutimiza wajibu wake katika kuandaa Sheria ambazo zimefanyiwa urekebu ili zitumike katika wakati sahihi.
Dkt Ndumbaro ameongeza kuwa Ofisi ya Mwandishi Mkuu wa Sheria (OCPD