Ikanga Speed aigomea Yanga | Mwanaspoti

KIUNGO Mshambuliaji, Jonathan Ikangalombo ‘Ikanga Speed’ aliyeingia Yanga kupitia dirisha, imetoa masharti mazito kwa mabosi wa klabu hiyo waliotaka kumtoa kwa mkopo kwenda Singida Black Stars.

Yanga ni kama bado haijamuelewa vya kutosha Ikanga Speed waliyemsajilui Januari mwaka huu akitokea AS Vita na hivyo, walikubaliana ikiwezekana wampeleke Singida akanoe makali zaidi na kupata nafasi ya kucheza zaidi, lakini menejimenti yake imechomoa juu ya mpango huo.

Inadaiwa kuwa, Ikanga Speed amewagomea mabosi wa klabu hiyo waliotaka kumtoa kwa mkopo kwenda Singida BS na badala yake anataka wamvunjie mkataba jumla na kumpa chake vinginevyo aendelee kusalia kikosini hapo.

Awali Mwanaspoti lilidokeza taarifa kwamba Yanga ilikuwa mbioni kumtoa kwa mkopo Ikanga Speed kutokana na kushindwa kufanya maajabu tangu alipotua akitokea AS Vita ya DR Congo, lakini inaelezwa nyota huyo wa zamani wa DC Motema Pembe pia ya DR Congo amewachomolea dili hilo.

Inadaiwa kuwa, wasimamizi wa mchezaji huyo, wameigomea Yanga kutaka kumtoa Ikanga Speed kwa mkopo kwenda popote na badala yake wanataka uvunjwe mkataba ili alipwe chake ili asepe jumla.

Chanzo hicho kilisema uongozi wa mchezaji huyo hautaki apelekwe kwa mkopo badala yake ulitaka uvunjwe mkataba wa miaka miwili uliyosalia, ili kila mmoja aendelee na maisha yake.

Kiungo mshambuliaji huyo anayemudu wingi zote mbili alijiunga na Yanga Janutai 16 mwakahuu kwa mkataba wa miaka miwili na nusu na tayari ameshatumikia nusu mwaka na imesalia miwili.

“Makubaliano yaliyofanyika hadi sasa ni Ikangalombo ataendelea kusalia Yanga, maana uongozi haupo tayari kuvunja mkataba wa miaka miwili kwani ingelazimika kulipa pesa ndefu, lakini usajili unaendelea lolote linaweza likatokea,” kilisema chanzo kutoka ndani ya Yanga na kuongeza;

“Yanga inaleta kocha mpya atakayekuja na machaguo yake na mifumo yake, hivyo kunaweza kukawa na mabadiliko ya kikosi akianza majukumu yake kila kitu kitakaa katika mstari, tutajua nani wanaondoka na nani wanaingia ila kwa sasa ni kwamba Ikangalombo bado yupo sana Jangwani.”

Tangu atuje Yanga, Ikangalombo amecheza mechi sita za Ligi Kuu akitumia dakika 136 akisti mara mbili, bila kufunga bao lolote, japo katika Kombe la Shirikisho (FA) alifunga moja katika hatua ya 16 Bora walipoifunga Songea United kwa mabao 2-0.

Kushindwa kuwika kwa mchezaji huyo kuliufanya uongozi wa Yanga kufikiria kuleta mbadala wake na ndipo hesabu za kumtoa kwa mkopo zilianza kwa nia ya kuletwa fundi wa kufunga mabao mengi na kutengeneza asisti nyingi kupitia pembeni kama walivyokuwa wakimpigia hesabu awali.

Related Posts