JKU Princess mabingwa Ligi ya Wanawake Zanzibar

KIKOSI cha JKU Princess, kimeibuka mabingwa wa Ligi Kuu Soka Wanawake Zanzibar (ZWPL) baada ya kuifunga Sauti Sisters mabao 2-0.

Wakati JKU Princess ikiwa bingwa wa ligi hiyo iliyoshirikisha timu nne, Warriors Queens imemaliza ligi hiyo bila kuvuna pointi hata moja.

Ligi hiyo imetamatika Alhamisi ya Julai 10, 2025 ulipochezwa mchezo huo ulioipa ubingwa JKU Princess kwenye Uwanja wa Mao B, Mjini Unguja.

Ushindi huo, umeifanya JKU Princess, kufikisha alama 16 ikiwa imecheza michezo sita kati ya hiyo imeshinda mitano na kutoa sare mmoja, ikifunga mabao 17 na kufungwa bao moja.

Sauti Sisters imemaliza nafasi ya pili kwa kucheza michezo sita ambapo imeshinda mitatu na kupoteza miwili huku ikitoka sare mchezo mmoja na kuvuna pointi 10, imefungwa mabao 10 na kufunga tisa.

Kwa upande wa Dunga Queens, imemaliza nafasi ya tatu kwa kushinda michezo mitatu na kupoteza mitatu, huku ikivuna alama 9, imefunga mabao 9 na kufungwa 19.

Warriors Queens imemalizika kwa kushika nafasi ya mwisho ya ligi hiyo ambapo ilipoteza michezo yote sita ikifunga mabao matano na kufungwa mabao 11.

Related Posts