Moto wateketeza Soko la Mashine Tatu Iringa, uchunguzi waendelea

‎Iringa. Soko maarufu la Mashine Tatu lililopo katika Manispaa ya Iringa limeteketea kwa moto usiku wa kuamkia leo Julai 12, 2025, ambapo vibanda na maduka kadhaa vimeteketea huku chanzo cha moto huo kikiwa bado hakijafahamika.

‎Mwananchi Digital ilifika katika eneo hilo alfajiri ya leo Jumamosi Julai 12, 2025 na kushuhudia moto ukiendelea kuwaka huku baadhi ya wafanyabiashara wa eneo hilo wakikusanyika kuangalia mali zao zikiendelea kuteketea.

‎Baadhi yao wamesema walipokea taarifa za moto saa nane usiku lakini juhudi za kuuzima zilikuwa ngumu kutokana na kuchelewa kuukabili.

‎Mamlaka husika za usalama zikiwemo Jeshi la Polisi na Kikosi cha Zimamoto tayari wapo eneo la tukio kwa uchunguzi wa awali huku wakiwahimiza wananchi kuendelea kuwa watulivu wakati taratibu za kubaini chanzo cha moto huo zikiendelea.

‎Kwa taarifa zaidi, endelea kufuatilia Mwananchi na mitandao yetu ya kijamii.

Related Posts