Beki KMC kutimkia JKT Tanzania

MABOSI wa JKT Tanzania wako kwenye hatua za mwisho kumalizana na beki wa mkongwe wa KMC, Fred Tangalo ambaye alimaliza mkataba na kikosi hicho msimu uliomalizika.

Beki huyo ambaye amewahi kuichezea Namungo, Lipuli na Polisi Tanzania, huku msimu uliomalizika ndio ulikuwa wa mwisho kwake ndani ya KMC.

Baada ya kutokuona dalili za kuendelea na kikosi hicho msimu ujao beki huyo alianza mazungumzo mapema na JKT Tanzania.

Taarifa kutoka kwa mtu wake wa karibu zinasema, Tangalo wakati wowote uongozi wake utamalizana na JKT Tanzania kwani pande hizo mbili ziko kwenye mazungumzo.

“JKT na uongozi wa Fred Tangalo uko katika hatua za mwisho kumaliza mazungumzo na haitakuwa ngumu kumpata kwa sababu hana mkataba na KMC,” chanzo kilisema.

KMC ilimaliza ligi nafasi ya 10 katika msimamo, ikiwa na pointi 35, ikishinda 9, sare 8 na kupoteza 13.

Related Posts