CHELSEA YACHUKUA UBINGWA WA DUNIA KWA VILABU 2025

 ::::::

Chelsea imetwaa Kombe la Dunia la Vilabu (WCW) baada ya kuichapa PSG mabao 3-0 katika Uwanja wa MetLife, Marekani. Mabao mawili ya Cole Palmer na Joao Pedro yametosha kuipa Chelsea ubingwa huo kwa mara ya pili katika historia yake.

 Licha ya matokeo kuwa mazuri kwa upande wa Chelsea waliutawala mchezo huo vipindi vyote viwili huku mwamuzi wa mchezo huo Alireza Faghan akitoa kadi tano katika mchezo huo.

 PSG walilazimika kumaliza pungufu mchezo huo baada ya kiungo wake, Joao Neves kumvuta nywele beki wa Chelsea Marc Cucurela. Kiungo wa Chelsea, Cole Palmer ametangazwa kuwa mchezaji bora wa fainali akifunga mabao mawili na kutoa pasi moja ya bao. 

FT: Chelsea 3-0 PSG.

Related Posts