Katibu wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Itikadi, Uenezi na Mafunzo . akiongea na Wandishi wa Habari leo tarehe 13 Julai 2025 katika Ofisi za Makao Makuu ya CCM Jijini Dodoma, amesema hakuna Mtia nia yeyote aliyeenguliwa kwenye nafasi za kuomba kugombea nafasi za Udiwani au Ubunge.
CPA. Makalla amesema mchakato bado unendelea ndani ya Chama na sasa Sekretarieti ya Chama hicho inaendelea kupokea taarifa kutoka Mikoani kisha kwenda Kamati kuu na baadae taarifa rasmi itawekwa wazi.
“Naomba nisisitize, kwa utaratibu wetu wa Chama cha Mapinduzi mpaka sasa hakuna Mtu ambaye ameenguliwa au kukatwa kama ambavyo inaripotiwa kwenye Vyombo vya Habari, nimeona ( wameandika ) huyu kapenya au huyu kafyekwa, huyu hayupo kwenye tatu bora, kama nilivyosema mchakato huu wa uteuzi utahitimishwa na kikao cha Kamati Kuu ya Chama cha Mapinduzi hapo ndio itakuwa mwisho wa kupata majibu ya mchakato mzima wa Wagombea wanaoteuliwa kwenda katika kura za maoni”
Aidha, CPA. Makalla amesisitiza kuwa mara baada ya Kamati Kuu kuketi na kujadili, CCM itatoka na kutoa taarifa rasmi ambazo ndizo za ukweli.
“Kamati Kuu itakapohitimisha tutatoka kuwaambia walioteuliwa kwenda katika kura za maoni ndani ya Chama cha Mapinduzi, zamani nyie mnajua ilikuwa Watu wote wakigombea wote wanakwenda kupigiwa kura za maoni kwahiyo tumesema utaratibu wa sasa watateuliwa wachache ili kwenda kupigiwa kura za maoni”