QS MUHONDA ATANGULIZA MBELE CCM


 :::::::::::

Mjumbe wa Mkutano Mkuu Taifa aliyemaliza Muda wake kuwakilisha Wilaya ya Kinondoni (Jumuiya ya Wazazi CCM), pia Mmilliki wa makampuni ya ‘QS Mhonda J Apex Group of Companies Ltd’ Joseph Boniface Mahonda (Mtia nia ya kugombea nafasi ya UBUNGE Jimbo la Kinondoni amewaasa wagombea wenzie wa Ubunge na wana CCM kwa ujumla kuwa watulivu kwenye mchakato wa ndani wa kuwapata wawakilishi wa CCM kwa ajili ya Uchaguzi wa mwezi Oktoba.

Mhonda, amesisitiza kwa kusema “Chama kwanza na Mtu baadae”

Usiri umetawala wa kinachoendelea ndani ya vikao vya Kamati za Siasa za Chama cha Mapinduzi (CCM) katika ngazi ya mikoa

vitakavyotoa mapendekezo ya kuwafyeka watiania 3,293 wa ubunge.

Kwa mujibu wa taarifa ya karibuni ya Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa CCM, Amos Makalla watiania wa nafasi ya ubunge katika majimbo 272 ya bara na visiwani wako 4,109, lakini Kamati za Siasa zinalazimika kutoa mapendekezo ya kukata majina 3,293 na kubaki majina 816 yakiwa matatu kwa kila jimbo kisha yatapendekezwa kwenye Kamati Kuu ya Halmashauri

Kuu ya CCM Taifa.

Related Posts