Lagos, Nigeria. Rais wa zamani wa Nigeria, Muhammed Buhari, amefariki dunia leo Julai 13, 2025 wakati akipatiwa matibabu jijini London.
Buhari aliyeiongoza Nigeria mara mbili kama mkuu wa jeshi na rais amefariki akiwa na umri wa miaka 82, Shirika la Habari la AP limemnukuu katibu wake wa habari, Bashir Ahmad leo Jumapili.
Kupitia akaunti yake ya X (zamani Twitter) Ahmad ameandika: “INNA LILLAHI WA INNA ILAIHIR RAJI’UN. Familia ya rais huyo wa zamani imetangaza kufariki kwa Muhammadu Buhari, GCFR, mchana wa leo katika kliniki moja mjini London. Mwenyezi Mungu ampokee katika Aljannatul Firdaus, Amin.”
Ikumbukwe Buhari aliingia madarakani mwaka 2015, akisimamia kipindi kibaya zaidi cha uchumi nchini humo na kupambana na uasi.
Kwa mujibu wa tovuti rasmi ya Ikulu ya Nigeria, Buhari alizaliwa Desemba 17, 1942, huko Daura, Jimbo la Katsina, Nigeria. Aliiingia jeshini akiwa na umri mdogo mwaka 1961 na kupata mafunzo nchini Nigeria, Uingereza, India na Marekani.
Katika kipindi chote cha utumishi wake jeshini, alishikilia nyadhifa mbalimbali muhimu za kamandi na wafanyakazi, akipanda vyeo na kufikia Meja Jenerali.
Alikuwa na jukumu katika mapinduzi ya kijeshi yaliyomuondoa Jenerali Yakubu Gowon madarakani mwaka 1975, na baada ya hapo aliteuliwa kuwa gavana wa kijeshi wa Jimbo la Kaskazini Mashariki (sasa Borno). Baadaye, alihudumu kama Kamishna wa Shirikisho wa Rasilimali za Petroli na Mwenyekiti wa Shirika la Taifa la Petroli la Nigeria (NNPC) kuanzia 1976 hadi 1978.
Lakini mnamo Desemba 31, 1983, Buhari alikuwa mkuu wa nchi wa kijeshi wa nchi hiyo baada ya mapinduzi yaliyoiangusha serikali ya kiraia ya Rais Shehu Shagari. Katika kipindi hiki, utawala wake ulijulikana kwa kampeni yake ya ‘Vita Dhidi ya Nidhamu’ (WAI), iliyolenga kupambana na rushwa na kukuza uzalendo.
Serikali yake pia ilijitahidi kukuza uchumi. Hata hivyo, utawala wake ulikosolewa kwa hatua za kukandamiza vyombo vya habari na uhuru wa kisiasa.
Alipinduliwa katika mapinduzi ya kijeshi yaliyoongozwa na Jenerali Ibrahim Babangida Agosti 1985 na baadaye alishikiliwa kwa miaka mitatu hadi 1988.
Baada ya kuachiliwa, Buhari aliteuliwa kuwa Mwenyekiti Mtendaji wa Mfuko wa Udhamini wa Petroli (PTF) mwaka 1994, akihudumu hadi 1999.
Aliingia katika siasa za kidemokrasia mnamo 2003, akigombea urais chini ya Chama cha All Nigeria Peoples Party (ANPP) bila mafanikio. Aligombea tena mwaka 2003, 2007 wakiwa na ANPP, na 2011 akiwa chini ya Congress for Progressive Change (CPC), chama alichosaidia kukianzisha.
Licha ya kushindwa mara kwa mara, alibaki kuwa mtu mashuhuri, mara nyingi akionekana kama asiyependa rushwa na mtetezi mkubwa dhidi ya rushwa.
Kutokata kwake tamaa kulimfanya kuwa rais kwani mwaka 2014, Buhari alikuwa mgombea urais wa chama kipya kilichoanzishwa cha All Progressives Congress (APC). Sifa yake ya uadilifu na historia yake ya kijeshi ziliwavutia Wanigeria wengi, hasa kutokana na wasiwasi kuhusu rushwa na ukosefu wa usalama.
Mnamo Machi 2015, alimshinda rais aliyekuwepo madarakani Goodluck Jonathan, ikiwa ni mara ya kwanza nchini humo rais aliyekuwapo madarakani kushindwa kwenye uchaguzi mkuu, ambapo Mei 29, 2015 aliapishwa kutumikia wadhifa huo.
Wakati wa muhula wake wa kwanza, utawala wake ulilenga kukabiliana na ukosefu wa usalama, kupambana na rushwa, na kufufua uchumi. Alizindua mipango kama vile Akaunti Moja ya Hazina (TSA) ili kuweka mapato ya Serikali katikati. Alichaguliwa tena kwa muhula wa pili mnamo Februari 2019, akimshinda Atiku Abubakar.
Muhula wake wa pili uliendelea kushughulikia changamoto za ukosefu wa usalama, hasa uasi wa Boko Haram, uharamia, na utekaji nyara, pamoja na masuala ya kiuchumi. Aliangushwa kwenye uchaguzi wa mwaka 2023 na rais wa sasa wa nchi hiyo Bola Tinubu, baada ya kuhudumu kwa mihula miwili kamili.