Benki ya NBC Yazindua Msimu wa Pili wa Kampeni ya NBC Shambani Kuhamasisha Kilimo cha Kahawa Mkoa wa Ruvuma.

Wakati wa hafla hiyo, Mkuu wa Kitengo cha Mikakati wa Benki NBC, Bw Msafiri Shayo aliwaongoza maofisa wengine wa benki hiyo akiwemo Meneja wa Benki ya NBC Kanda ya Pwani Bi Zubeider Haroun na Mkuu wa kitengo cha wateja wadogo wadogo na wakulima kutoka Benki ya NBC, Bw Raymond Urassa .

Akizungumzia kampeni hiyo, DC Makori pamoja na kuipongeza benki hiyo kwa kutoa kipaumbele kwa wakulima nchini kupitia huduma zake, alisema ujio wa kampeni hiyo wilayani mwake ni ukombozi muhimu kwa wakulima wa kahawa wanaohitaji upendeleo maalum wa huduma za kifedha na kwamba serikali imejipanga kuhakikisha dhamira ya benki hiyo inafanikiwa.

“Zaidi nimefurahi kusikia kupitia kampeni hii wakulima wanaweza kupata mikopo ya vitendea kazi muhimu kama vile matrekta na zana nyingine za kisasa za kilimo, pembejeo za kilimo na mikopo ya malipo ya awali kwa wakulima.’’

“Pia huduma za bima za afya na kilimo zinazotolewa na NBC ni muhimu sana kwa wakulima, hasa katika kukabiliana na changamoto za kiafya kwao binafsi na familia zao na kujilinda dhidi ya hasara zitokanazo na majanga ya asili ambayo yamekuwa yakiathiri mazao yao,’’ alisema.

Akizungumza kwenye hafla hiyo, Bw Msafiri alisema kampeni hiyo ni sehemu ya muitikio wa benki ya NBC kufuatia wito wa Serikali wa kuchangia katika kufanikisha agenda 10/30 ya kuongeza uzalishaji wa mazao ya kilimo kutoka asilimia 5 hadi 10 ifikapo mwaka 2030.

“Sambamba na uzinduzi wa kampeni hii kwa wakulima wa zao la kahawa wilayani mbinga, pia tunatoa huduma mbali mbali kwao ikiwemo, ufunguaji wa akaunti za wakulima, ambazo hazina makato ya mwezi, huduma za mikopo kwa mkulima mmoja mmoja kwa ajili ya zana za kilimo kama matrekta na mikopo kwa vyama vya ushrika (AMCOS/Union) kwa ajili ya pembejeo zao.’’ Alitaja.

Kupitia kampeni hiyo benki ya NBC inatoa huduma za bima ya afya kwa wakulima na huduma za bima ya kilimo inayotoa fursa kwao kulipwa fidia pindi mazao yao yatakapoathiriwa na majanga mbalimbali yakiwemo yale ya asili.

Akifafanua zaidi kuhusu kampeni hiyo Bw Urassa alisema inawalenga wakulima wote wakiwemo mmoja mmoja, vyama vikuu vya ushirika na vyama vya msingi (AMCOS) ambavyo vitapitisha fedha za mauzo kwenye akaunti za NBC Shambani.

“Kupitia kampeni hii ambayo kwa mwaka huu tunaizindua kwa mara ya pili hapa mkoani Ruvuma mahususi kwa wilaya za Mbinga na Nyasa, wakulima wataweza kujishindia vitendea kazi mbali mbali kama vile ‘spray pumps’ ( pampu ya kupulizia dawa) na piki piki. Upande wa AMCOS na UNION watapata fursa ya kujishindia maguta kwa ajili ya usafirishaji wa mazao yao.’’ Alitangaza.

Wakizungumza kwa niaba wakulima hao, Mwenyekiti wa AMCOS ya Kibandai Bi Vestina Nombo pamoja nae Katibu wa Kipowolo AMCOS Bw Matius Kapinga pamoja na kuishukuru na kuipongeza benki hiyo kwa kampeni hiyo muhimu, walionyesha kuvutiwa na huduma za bima za afya na bima za kilimo kutokana na hitaji kubwa walilonalo wakulima hao kwenye masuala huduma bora za kiafya kwa ajili yao na familia zao huku pia wakiitaja huduma ya bima ya kilimo kama suluhisho sahihi dhidi ya athari zitokanazo na majanga mbalimbali yanayoathiri mazao yao.

Mkuu wa Wilaya ya Mbinga, Bw Kisare Makori (Katikati) akikata utepe kuashiria uzinduzi wa kampeni ya ‘Shinda Mechi Zako Kinamna Yako na NBC Shambani’ inayoratibiwa na benki ya NBC mahususi kwa wakulima wa zao la kahawa wilaya za Mbinga na Nyasa mkoa wa Ruvuma. Uzinduzi huo uliofanyika mwishoni mwa wiki wilayani Mbinga. Wengine ni pamoja na Mkuu wa Kitengo cha Mikakati wa Benki NBC, Msafiri Shayo (wa nne kulia), Meneja wa Benki ya NBC Kanda ya Pwani Bi Zubeider Haroun (wa tatu kushoto) maofisa wengine wa benki hiyo pamoja na wadau wa kilimo mkoani Ruvuma wakiwemo wakulima.

Mkuu wa Wilaya ya Mbinga, Bw Kisare Makori (alieshika mic) akizunguza na wageni waalikwa wakiwemo wadau wa sekta ya kilimo mkoani Ruvuma na maofisa wa benki ya NBC wakati wa hafla ya uzinduzi wa kampeni ya ‘Shinda Mechi Zako Kinamna Yako na NBC Shambani’ inayoratibiwa na benki ya NBC mahususi kwa wakulima wa zao la kahawa wilaya za Mbinga na Nyasa mkoa wa Ruvuma. Uzinduzi huo uliofanyika mwishoni mwa wiki wilayani Mbinga.

Mkuu wa Wilaya ya Mbinga, Bw Kisare Makori (alievaa tai) akiwa kwenye picha ya pamoja na wageni waalikwa wakiwemo wadau wa sekta ya kilimo mkoani Ruvuma na maofisa wa benki ya NBC wakati wa hafla ya uzinduzi wa kampeni ya ‘Shinda Mechi Zako Kinamna Yako na NBC Shambani’ inayoratibiwa na benki ya NBC mahususi kwa wakulima wa zao la kahawa wilaya za Mbinga na Nyasa mkoa wa Ruvuma. Uzinduzi huo uliofanyika mwishoni mwa wiki wilayani Mbinga.

Mkuu wa Kitengo cha Mikakati wa Benki NBC, Bw Msafiri Shayo (alieshika mic) akizungumza na wageni waalikwa wakiwemo wadau wa sekta ya kilimo mkoani Ruvuma wakati wa hafla ya uzinduzi wa kampeni ya ‘Shinda Mechi Zako Kinamna Yako na NBC Shambani’ inayoratibiwa na benki ya NBC mahususi kwa wakulima wa zao la kahawa wilaya za Mbinga na Nyasa mkoa wa Ruvuma. Uzinduzi huo uliofanyika mwishoni mwa wiki wilayani Mbinga.

Meneja wa Benki ya NBC Kanda ya Pwani Bi Zubeider Haroun (alieshika mic) akizungumza na wageni waalikwa wakiwemo wadau wa sekta ya kilimo mkoani Ruvuma wakati wa hafla ya uzinduzi wa kampeni ya ‘Shinda Mechi Zako Kinamna Yako na NBC Shambani’ inayoratibiwa na benki ya NBC mahususi kwa wakulima wa zao la kahawa wilaya za Mbinga na Nyasa mkoa wa Ruvuma. Uzinduzi huo uliofanyika mwishoni mwa wiki wilayani Mbinga.

Mkuu wa kitengo cha wateja wadogo wadogo na wakulima kutoka Benki ya NBC, Bw Raymond Urassa (alieshika mic) akizungumza na wageni waalikwa wakiwemo wadau wa sekta ya kilimo mkoani Ruvuma wakati wa hafla ya uzinduzi wa kampeni ya ‘Shinda Mechi Zako Kinamna Yako na NBC Shambani’ inayoratibiwa na benki ya NBC mahususi kwa wakulima wa zao la kahawa wilaya za Mbinga na Nyasa mkoa wa Ruvuma. Uzinduzi huo uliofanyika mwishoni mwa wiki wilayani Mbinga.

Maofisa mbalimbali wa benki ya NBC wakielezea kuhusu huduma mbalimbali za benki hiyo mahususi kwa wakulima mbele ya wageni waalikwa wakiwemo wadau wa sekta ya kilimo mkoani Ruvuma wakati wa hafla ya uzinduzi wa kampeni ya ‘Shinda Mechi Zako Kinamna Yako na NBC Shambani’ inayoratibiwa na benki ya NBC mahususi kwa wakulima wa zao la kahawa wilaya za Mbinga na Nyasa mkoa wa Ruvuma. Uzinduzi huo uliofanyika mwishoni mwa wiki wilayani Mbinga.


Wakiwa kwenye hafla ya uzinduzi huo wakulima walipata wasaa wa kuuliza maswali mbalimbali kuhusu huduma mbalimbali zinazotolewa na benki ya NBC kwa ajili yao.


Muonekano wa baadhi ya zawadi zitakazotolewa kwa washindi mbalimbali wa kampeni hiyo.

Related Posts