Burkina Faso yataja 25 kuivaa Stars CHAN

JOTO la fainali za michuano ya Kombe la Mataifa Afrika kwa Wachezaji wa Ndani (CHAN), linazidi kupanda taratibu ambapo Burkina Faso imetaja wachezaji 25 watakaoshiriki kwenye fainali hizo.

Burkina Faso ambayo itacheza mchezo wa kwanza wa ufunguzi dhidi ya wenyeji Tanzania, Agosti 2 mwaka huu ukiwa ni wa kundi B, kwenye kikosi chake imewajumuisha makipa watatu, mabeki sita, viungo saba na washambuliaji tisa.

Kwenye orodha hiyo ya wachezaji wa kocha Issa Balbone, makipa ni Ladji Sanou(AS Sonabel), Mathieu Konvelbo (Rahimo FC) na Moussa Traore (ASFB).

Mabeki ni Patrick Malo, Abbas Guirro (wote USFA), Enock Belem (Majestic SC), Christophe Ouattara (Rahimo FC), Walid Guira(AS Sonabel), Andalou Sagne(AS Douane).

Viungo wamo Khalifa Nikiema (AS Douane), Moumoune Diallo (Sporting Cascade), Abdoulaye Toure (ASFA Yennenga), Tertus Bagre (Real du Faso), Frank Aime Tologo (Vitesse  FC), Cedric Barro (Rahimo FC) na Adjibade Chitou (Real du Faso).

Balbone amewaita washambuliaji Damassi Konate (AS Sonabel), Ousmane Sirri (ASFB), Ramain Atiou (AS Sonabel), Karim Baguian (USFA), Souleymane Sangare (Sporting Cascade), Issouf Kabore(Majestic FC), Eliazar Ouattara (Majestic FC), Ives Koutiama (USFA) na Papus Ouattara(Vitesse FC).

Kundi B la michuano hiyo mbali na Tanzania na Burkina Faso, timu zingine ni Madagascar, Mauritania na Jamhuri ya Afrika ya Kati.

Related Posts