Kumradhi Nehemiah Mchechu | Mwananchi

Kampuni ya Mwananchi Communications Limited, wachapishaji wa magazeti ya Mwananchi, The Citizen, na Mwanaspoti, inaomba radhi kwa Nehemiah Kyando Mchechu kutokana na makala iliyochapishwa katika toleo Na. 4551 la gazeti la The Citizen Ijumaa la Machi 23, 2018.

Tunakiri kuwa habari hiyo ilikuwa na tuhuma ambazo zimebainika kuwa za kudhalilisha dhidi ya Mchechu na ilikuwa na upungufu kitaaluma.

Kwa sababu hiyo, tunaomba radhi kwa usumbufu, madhara na fedheha iliyosababishwa na taarifa hiyo.

Related Posts