MKOA WA TANGA WAPOTEZA SHILINGI BILION 2

………….

NA Ester Maile Dodoma 

Mkoa wa Tanga wapoteza kiasi cha shilingi Bilioni 2 kufuatia wawekezaji wa Kampuni za Saruji kugomea tozo ya mazao ya madini Mkoani hapo Mgogoro ambao bado unashugulikiwa na Mkoa huo 

Hayo yamebainishwa na Mkuu wa mkoa wa Tanga Dkt Batilda Burian leo 15 julai 2025 jijini Dodoma wakati akizungumza na waandishi wa habari akielezeea mafanikio ya mkoa huo ndani ya miaka minne ya uongozi wa serikali ya awamu ya sita.

Burian ameongeza kuwa mashamba ya liyotelekezwa yataanza kufatiliwa kwani walioyachukua mashamba hayo walichukua kwa lengo la kupatia mikopo nje ya nchi. 

Hata hivyo mkoa wa Tanga unampango na dhamira ya dhati ya zao la machungwa ambapo.yanazalishwa kwa wingi katika mkoa hu ambapo kuanzia maganda ya chungwa yanauzwa na kuongeza pato katika mkoa huu.

 

Related Posts