Nondo achukua fomu ya ubunge, aingia anga za Zitto

Kigoma. Kiongozi wa Ngome ya Vijana Taifa Chama cha ACT-Wazalendo, Abdul Omary Nondo, maarufu Abdul Nondo, amechukua fomu ya kuomba kuteuliwa na chama chake kugombea ubunge Jimbo la Kigoma Mjini katika Uchaguzi Mkuu ujao.Nondo amekabidhiwa fomu hiyo leo, Julai 15, 2025, na Katibu wa chama hicho wa Jimbo la Kigoma Mjini, Idd Adamu.Hii ni mara yake ya pili kutangaza nia ya kugombea ubunge katika jimbo hilo, ambapo, kama ilivyokuwa katika Uchaguzi Mkuu wa 2020, atachuana tena na mbunge wa zamani wa jimbo hilo, Zitto Kabwe, ambaye alichukua fomu mapema Aprili 18, 2025.Akizungumza mara baada ya kukabidhiwa fomu, alisema:”Naamini safari hii wajumbe na chama changu watanipa ridhaa ya kupeperusha bendera katika jimbo hili, kwa lengo la kurejesha hadhi ya Kigoma Mjini.“Jimbo hili si sehemu ya kutafuta sifa wala umaarufu; watu wa Kigoma wana uelewa wa kutosha na wanajua ni nani anayefaa kuwaongoza.” Historia yakeNondo ni mwanasiasa na kiongozi wa vijana wa chama cha ACT‑Wazalendo (Ngome ya Vijana). Amejulikana kutokana na uongozi wake wa vijana.Pia, amefahamika kwa kuongoza kampeni na kuendesha siasa za vijana pamoja na kusisitiza umuhimu wa katiba imara na demokrasia ndani ya Tanzania.Nondo anapambana ndani ya kura za maoni za chama hicho na Zitto Kabwe ambye ni kiongozi mstaafu wa ACT‑Wazalendo na mbunge wa zamani wa Jimbo la Kigoma Mjini, (2005–2015).Pia, Zitto akiwa bungeni aliongoza Kamati ya Hesabu za Umma (PAC), akijitolea kupambana na rushwa na kuimarisha uwajibikaji wa matumizi ya fedha za umma.Zitto ni mwanzilishi wa ACT‑Wazalendo mwaka 2015 baada ya kuondoka Chadema, na ameongoza chama hicho hadi Machi 2024, akiwekeza nguvu katika demokrasia, uwazi na demokrasia ya serikali.

Related Posts