Askofu Gwajima Ataka Mfumo wa Uchaguzi Kubadilishwa – Global Publishers



Askofu Gwajima

Askofu Gwajima Ataka Mfumo wa Uchaguzi Kubadilishwa Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima ambaye pia ni Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, Josephat Gwajima, amekitaka Chama cha Mapinduzi (CCM) na Serikali kutumia muda mfupi uliosalia kabla ya kuvunjwa kwa Bunge kutekeleza mabadiliko ya msingi ya uchaguzi (reforms) ili kuhakikisha Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kinashiriki uchaguzi mkuu wa Oktoba 2025.

Akizungumza kupitia video aliyochapisha mtandaoni siku ya leo Jumatano, Askofu Gwajima amesema kwamba kwa maslahi ya taifa ni muhimu kufanya marekebisho machache ya kisheria ambayo hayahitaji muda mrefu ili “CHADEMA waingie, halafu tuwapige “.

Gwajima amesema kuwa kushinda uchaguzi pasipo kushirikisha vyama vyote muhimu si ushindi wa busara, kwani utaleta utawala wa migogoro na kutishia mshikamano wa kitaifa huku akiwataka WanaCCM na serikali kuangalia mbali zaidi ya ushindi wa kisiasa na kufikiri namna ya kujenga taifa lenye maridhiano baada ya uchaguzi. “Haitapendeza baada ya uchaguzi taifa litawaliwe na maandamano maaskari wawe wanapambana na waandamanaji,” amsema Askofu Gwajima.

 


Related Posts