BDL iko juu zaidi ya ligi ya Congo

Nyota wa Savio, Ntibonela Bukeng amekiri Ligi ya mpira wa Kikapu Dar es Salaam (BDL), iko juu zaidi ya ligi ya DR Congo.

Bukeng aliliambia Mwanaspoti ubora huo umetokana na ushindani mkubwa unaoonyeshwa na timu zote shiriki.

Bukenge ambaye ni raia wa Congo, alitoa ushauri kwa chama cha mchezo huo Dar es Salaam (BD), kuendelea kuboresha ligi hiyo  zaidi ili nao waweze kushawishika zaidi.

“Ubora umefanya wachezaji wengi wa Congo washawishike kutaka kucheza BDL,” alisema Bukenge.

Wakati huo huo, Savio iliifunga Pazi kwa pointi 78-77, katika mchezo mkali na wa kusisimua kwenye Uwanja wa Donbosco Upanga.

Baadhi ya wachezaji walionyesha viwango katika mchezo huo  kutoka Pazi ni Josephat Petar, Soro Geofrey, Isaya Mwamaja na Ethani Jamego, huku kwa Savio ni Oscar Mwituka, Cornelius Mgaza, Godfrey Swai na Ntibonela Bukeng.

Katika mchezo huo, Bukeng aliongoza kwa kufunga pointi 29,  akifuatiwa na Mgaza pointi 16 na kati ya hizo alifunga eneo la mtupo mmoja wa ‘three pointi’ 12.

Related Posts